Maonyesho ya Bidhaa za Kiafrika katika Mkutano Mkuu na Baraza wa Mashirika ya Viwango Afrika (ARSO)

20 – 24 JUNI, 2016 ARUSHA

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF) , wanawaalika wazalishaji wote kujiandikisha kushiriki katika Mashindano ya Bidhaa 50 Bora zinazozalishwa Tanzania na katika Maonesho ya Bidhaa za Kiafrika “ARSO Made in Africa Expo” ambayo yatafanyika jijini Arusha kuanzia Juni 20 hadi 24,2016.

Mashindano hayo ni sehemu ya maandalizi ya Maonesho ya Bidhaa Bora za Kiafrika yanatakayofanyika katika ngazi ya bara nchini Misri mwaka 2017.

Ushiriki katika Maonesho hayo ni fursa na jukwaa la kujenga mtandao wa maingiliano baina ya Jumuiya ya Wafanyabiashara na wazalishaji wa bidhaa kutoka nchi mbalimbali barani Afrika,  kuvutia wawekezaji katika sekta ya viwanda na kupata muda kuonesha bidhaa wakati wa Mkutano Mkuu na Baraza la ARSO.

Kwa mara ya kwanza, kupitia Shirika la Viwango Tanzania, mwaka huu Tanzania ndio mwenyeji wa Mkutano Mkuu na Baraza la ARSO. Mkutano huo utahudhuriwa na wageni kutoka nchi 37 za Afrika na wahisani wa maendeleo kutoka ndani na nje ya bara la Afrika.


Kwa mawasiliano zaidi:
Mkurugenzi Mkuu,
Shirika la Viwango Tanzania,
S. L.P 9524,
Dar es Salaam
Barua pepe: .(JavaScript must be enabled to view this email address),
Tovuti: http://www.tbs.go.tz
255 (22) 2450206/2450949
Simu: 0782931197 (Gladness), 0786476284 (Jane-TPSF)


Tafadhali bonyeza linki ifuatayo ili uweze kulipata hili tangazo:

Maonyesho_ya_Bidhaa_za_Kiafrika_katika_Mkutano_Mkuu_na_Baraza_wa_Mashirika_ya_Viwango_Afrika.pdf

Tafadhali bonyeza linki ifuatayo ili uweze kuchukua fomu ya usajili:

ARSO_MADE_IN_AFRICA_EXPO_Registration_Form_2016.docx