MFUMO WA ULIPAJI KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI


Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linapenda kuutarifu umma kuwa limejiunga kwenye mfumo wa Serikali wa malipo ya kielekroniki kwa kuzingatia matakwa ya Sheria ya Fedha za Umma ya 2017 yanavyoelekeza kuwa fedha zote za umma zinapaswa kukusanywa kupitia mfumo wa serikali wa malipo ujulikanao kama Government e-Payment Gateway (GePG). Ili kwenda sanjari na mfumo wa Serikali, TBS imetengeneza mfumo wa malipo wa kielektroniki (Electronic Payment System, ePS) ambao umeunganishwa na mfumo wa serikali (GePG). Mfumo huu mpya wa malipo wa TBS (ePS) uliingizwa rasmi katika matumizi tarehe 10 Januari, 2018 kwa ofisi za TBS zilizoko Dar es Salaam.

Kwa Maelezo zaidi fungua “Link”  ifuatayo

MFUMO_WA_ULIPAJI_KWA_NJIA_YA_KIELEKTRONIKI.pdf