SEMINA KWA WAAGIZAJI WA BIDHAA KUTOKA NJE YA NCHI NA MAWAKALA WA FORODHA WA MKOA WA DAR ES SALAAM

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linawatangazia waagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi na Mawakala wa Forodha kuwa limeandaa semina ya mafunzo ya udhibiti ubora wa bidhaa itakayofanyika tarehe 20 na 21 Februari, 2017 katika ukumbi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) jengo la Mafao lililopo Ilala Dar es Salaam, kuanzia saa tatu (3) kamili asubuhi mpaka saa tisa (9) alasiri

Lengo la semina hii ni kutoa mafunzo kwa walengwa juu ya taratibu za ukaguzi wa bidhaa nje ya nchi kabla ya kusafirishwa kuja nchini yaani Pre-shipment Verification of Conformity to Standards (PVoC) na zile zinazokaguliwa baada ya kufika nchini.

Washiriki wanatakiwa kujiorodhesha majina yao kwenye sehemu zifuatazo:

1. Ofisi za Jumuiya ya Wafanyabiashara zilizopo Kariakoo
2. Ofisi za Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFFA) zilizopo eneo la Gerezani
3. Ofisi za TBS zilizopo jengo la Diplomat lililopo mtaa wa Kaluta/Mkwepu, Posta
4. Ofisi za TBS Makao Makuu zilizopo Ubungo, Dar es Salaam.

Mwisho wa kujiandikisha ni Ijumaa tarehe 17 – 02 – 2017 saa kumi kamili jioni. Zingatia kuwa watakaojiandikisha ndio watakaoshiriki semina hiyo.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na:

Mkurugenzi Mkuu,
Shirika la Viwango Tanzania,
S.L.P. 9524,
Dar es Salaam,
Simu: +255(022) 2450206
Hotline: +0800110827
Barua pepe: .(JavaScript must be enabled to view this email address)

                         
                                      WOTE MNAKARIBISHWA


Tafadhali bonyeza linki ifuatayo ili uweze kupakua tangazo hili:
Tangazo_la_Semina_-_Feb_2017.pdf