SEMINA KWA WATENGENEZAJI, WAAGIZAJI, WASAMBAZAJI NA WADAU WA BIDHAA ZA NONDO

image
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linapenda kuwafahamisha watengenezaji, waagizaji, wasambazaji na wadau wa bidhaa za nondo kuwa tarehe 29-08-2019 kuanzia saa 2:30 asubuhi hadi saa 7:00 mchana kutakuwa na semina itakayofanyika Makao Makuu ya Shirika la Viwango Tanzania, Ubungo, Dar es Salaam.

Semina hii inalenga kutoa elimu juu ya matakwa ya Viwango vya nondo, utaratibu wa uingizaji na uthibitishaji wa bidhaa hizi, matumizi ya mfumo wa kuomba huduma kwa njia ya mtandao pamoja na kujadili changamoto zilizopo kwenye soko kwa sasa kuhusiana na bidhaa hizi.

Kwa taarifa hii watengenezaji, waagizaji, wasambazaji na wadau wa bidhaa za nondo mnaombwa kuhudhuria semina hii muhimu .

Kwa taarifa zaidi wasiliana na:
Mkurugenzi Mkuu,
Shirika la Viwango Tanzania,
S L P 9524, Dar es Salaam.
Simu: +255 (022) 2450298; Hotline: +0800 110 827
Barua pepe: .(JavaScript must be enabled to view this email address); Tovuti: http://www.tbs.go.tz

Kwa Maelezo Zaidi bofya hapa

SEMINA_KWA_WATENGENEZAJI,_WAAGIZAJI,_WASAMBAZAJI_NA_WADAU_WA_BIDHAA_ZA_NONDO.pdf