SEMINA KWA WAZALISHAJI, WAAGIZAJI, WASAMBAZAJI NA WAUZAJI WA BIDHAA ZA UMEME NURU

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kushirikiana na taasisi inayoshughulikia masuala ya fedha (IFC) limeandaa semina kwa wadau wote wa umeme nuru itayowahusisha wazalishaji, waagizaji, wasambazaji na wauzaji wa bidhaa za umeme nuru. Semina hiyo itafanyika tarehe 2018-03-21 kuanzia saa tatu (03.00) asubuhi mpaka saa saba (07.00) kamili mchana katika ofisi za TBS Makao Makuu zilizopo Ubungo jijini Dar es Salaam.

image

Katika Semina hiyo elimu kuhusu utekelezaji wa viwango vya bidhaa husika kama ilivyoainishwa katika viwango vya lazima vya kitaifa TZS 1951:2017 na TZS 1952 - 9- 5:2017 itatolewa, ili waagizaji, wasambazaji na wauzaji wa bidhaa za umeme nuru waweze kufuata na kutekeleza matakwa ya lazima ya viwango husika.
Washiriki wanatakiwa kujiorodhesha majina yao kwenye Ofisi za TBS Makao makuu, zilizopo Ubungo na ofisi za TBS zilizopo jengo la Diplomat, mtaa wa Kaluta/Mkwepu Posta. Mwisho wa kujiandikisha ni Jumatano tarehe 2018-03-16 saa kumi kamili (10) jioni.

Zingatia kuwa watakaojiandikisha ndio watakaoshiriki katika semina hiyo.
Tafadhali bonyeza linki ifuatayo kupata tangazo hili:

*Tangazo:UMEME_NURU_SEMINA_ONE.pdf