SEMINA KWA WAZALISHAJI, WAKANDARASI, WASAMBAZAJI NA WAAGIZAJI WA NYAYA ZA UMEME

image
Shirika la viwango Tanzania (TBS) linawatangazia kuwa limeandaa semina kwa ajili ya wazalishaji, wakandarasi, wasambazaji na waagizaji wa nyaya za umeme itakayofanyika tarehe 21 Septemba 2017 kuanzia saa tatu (3) asubuhi mpaka saa saba (7) kamili mchana katika ofisi za TBS zilizopo Ubungo jijini Dar es Salaam.

Lengo la semina hii ni kutoa mafunzo jinsi ya utekelezaji wa mabadiliko ya rangi za nyaya za umeme kama ilivoainishwa katika kiwango cha TZS 1518:2015 ili kuwezesha wazalishaji na wafanya wa ndani na nje na kufuata matakwa ya kiwango husika.
Washiriki wanatakiwa kujiorodhesha majina yao kwenye Ofisi za TBS Makao makuu zilizopo Ubungo Dar es Salaam na ofisi za TBS zilizopo jengo la Diplomat lililopo mtaa wa Kaluta/Mkwepu Posta. Mwisho wa kujiandikisha ni jumatano tarehe 20 .09.2017 saa kumi kamili jioni.
Zingatia kuwa watakaojiandikisha ndio watakaoshiriki semina hiyo.

Kwa maelezo Zaidi wasiliana na:
Mkurugenzi mkuu
Shirika la Viwango Tanzania (TBS)
S.L.P 9524
Dar es Salaam
Simu: +255(022)2450206
Hotline: +0800110827
Barua pepe: .(JavaScript must be enabled to view this email address)

<>Kwa maelezo zaidi bofya hapa
TANGAZO_LA_SEMINA_.pdf