TAARIFA KWA UMMA

UKAGUZI WA MAGARI YALIYOTUMIKA KUTOKA UINGEREZA

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linapenda kuuarifu umma kuwa limefuta leseni Na. 0655 iliyotolewa kwa Kampuni ya WTM Utility Services Ltd, Unit 19, Coldharbour House, Coldharbour Lane, Rainham, Essex, RM13 9YA, UK kwa ajili ya kukagua magari yaliyotumika yanayoingizwa nchini kutoka Uingereza. Leseni hiyo imefutwa kuanzia tarehe 18-06-2012.

Kwa taarifa hii, tunapenda kuwaasa waagizaji wote wa magari yaliyotumika kutoka Uingereza kukagua magari yao kupitia kampuni ya Vehicle Operator Services Agency (VOSA).  Magari yote yatakayoletwa nchini kutoka Uingereza bila kuwa na cheti halali cha ukaguzi kutoka Vehicle Operator Services Agency (VOSA) hayataruhusiwa kuingia katika soko la Tanzania.

Kwa maelezo zaidi, wasiliana na:

Mkurugenzi Mkuu
Shirika la Viwango Tanzania
S L P 9524
DAR ES SALAAM

Simu: 255 22 2450298/2450206/24517636
Faksi: 255 22 2450959
Baruapepe: .(JavaScript must be enabled to view this email address)