TAARIFA KWA UMMA

UKAGUZI WA MAGARI YALIYOTUMIKA KUTOKA DUBAI

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linapenda kuuarifu umma kuwa limefuta leseni Na. 0656 iliyotolewa kwa Kampuni ya Jaffar Mohammed Ali Garage ya S L P 60329, DUBAI, Falme za Kiarabu (U.A.E), kwa ajili ya kukagua magari yaliyotumika yanayoingizwa nchini kutoka Dubai. Leseni hiyo imefutwa kuanzia tarehe 18-06-2012.

Kwa taarifa hii, tunapenda kuwaasa waagizaji wote wa magari yaliyotumika kutoka Dubai kukagua magari yao kupitia kampuni ya Jabal Kilimanjaro Auto Elect Mechanical ya S L P 68232, Sharjah, Falme za Kiarabu (U.A.E).  Magari yote yatakayoletwa nchini kutoka Dubai bila kuwa na cheti halali cha ukaguzi kutoka Jabal Kilimanjaro Auto Elect Mechanical ya S L P 68232 Sharjah, Falme za Kiarabu (U.A.E.) hayataruhusiwa kuingia katika soko la Tanzania.

Kwa maelezo zaidi, wasiliana na:
Mkurugenzi Mkuu
Shirika la Viwango Tanzania
S L P 9524
DAR ES SALAAM

Simu: 255 22 2450298/2450206/24517636
Faksi: 255 22 2450959
Baruapepe: .(JavaScript must be enabled to view this email address)