TAARIFA KWA UMMA

KUHAMA KWA OFISI YA UDHIBITI WA SHEHENA

Tunapenda kuwaarifu wateja wetu pamoja na umma kwa ujumla kuwa kuanzia tarehe 16 Julai, 2012, huduma zote za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) zinazohusiana na shehena zinazoingia nchini kutoka nje ya nchi zitahamia katika ofisi mpya zilizoko katika anwani ifuatayo:

Samora House, Ghorofa ya Nne
Mtaa wa Samora
Katika jengo linalotumiwa pia na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Dar es Salaam.

Huduma zitakazohama ni pamoja na zile zinazohusiana na:
• Ukaguzi wa bidhaa katika nchi zinakotoka kabla hazijasafirishwa kuja nchini (PVoC);
• Ukaguzi wa magari yaliyotumika kabla ya kuingizwa nchini;
• Ukaguzi wa shehena mipakani;
• Udhibiti wa shehena za vimiminika (wet cargo);
• Huduma zote za ukaguzi wa bidhaa zinazoingizwa nchini kutoka nchi mbalimbali.

Ni matarajio yetu kuwa utahudumiwa vema na kwa haraka zaidi katika ofisi zetu hizi mpya.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
Mkurugenzi Mkuu
Shirika la Viwango Tanzania
S L P 9524
DAR ES SALAAM

Simu: 255 22 2450298/2450206
Faksi: 255 22 2450959
Baruapepe: .(JavaScript must be enabled to view this email address)