TAARIFA KWA UMMA

UTEKELEZAJI WA MPANGO WA KUKAGUA BIDHAA KATIKA NCHI ZINAKOTOKA KABLA HAZIJASAFIRISHWA KUJA NCHINI (PVoC)

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) lilianza kukagua na kuthibitisha ubora wa bidhaa katika nchi zinakotoka kabla hazijasafirishwa kuja nchini kuanzia Februari 1, 2012. Utaratibu huu unafanyika chini ya Mpango wa Kuthibitisha Ubora wa Bidhaa katika nchi zinakotoka kabla hazijasafirishwa kuja nchini (PVoC).

TBS inapenda kuwakumbusha waagizaji wote wa bidhaa kutoka nchi za nje pamoja na umma kwa ujumla kuwa shehena zote zinapaswa kuthibitishwa kuwa zinakidhi matakwa ya viwango husika kabla hazijasafirishwa kuja Tanzania. Shehena zitakazokidhi matakwa ya ubora zitapewa Cheti cha Ubora (CoC).

Kuanzia Agosti 1, 2012, shehena zote zisizo na CoC zitatozwa faini ya asilimia kumi na tano (15%) ya thamani ya CIF kisha kukaguliwa kwa utaratibu wa ukaguzi wa bidhaa zinapoingia, yaani Destination Inspection. Shehena zisizokidhi matakwa ya viwango zitarejeshwa katika nchi zinakotoka au kuharibiwa kwa gharama ya mwagizaji.

Ili kuepuka kadhia hii, waagizaji wote wa bidhaa wanaaswa kuhakikisha kuwa shehena zao zinathibitishwa na mawakala wa ukaguzi wa TBS ambao wana ofisi kote duniani. Mawakala hao ni:

1) Intertek
2) Bureau Veritas
3) SGS

Maelezo zaidi kuhusiana na mawakala wa TBS pamoja na ofisi zao duniani kote yanapatikana katika tovuti yetu, http://www.tbs.go.tz.


Kwa maelezo zaidi wasiliana na:

Mkurugenzi Mkuu
Shirika la Viwango Tanzania
S L P 9524
DAR ES SALAAM
Simu: 255 22 2450298/2450206
Faksi: 255 22 2450959
Baruapepe: .(JavaScript must be enabled to view this email address)

Tafadhali bofya linki ifuatayo ili uweze kupata tangazo hili kwa matumizi yako:

Taarifa_kwa_Umma_Utekelezaji_wa_PVoC