TAARIFA KWA UMMA

image
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linatambua kuwa ni vyema kuwe na jitihada mahususi kwa ajili ya wafanyabiashara ili kuwakwamua na kuwasaidia waweze kusafirisha bidhaa zenye ubora na kukidhi matakwa ya viwango ili kuweza kupata masoko ya ndani na nje ya nchi hivyo kuchochea ukuaji wa sekta ya viwanda hapa nchini.

TBS inapenda kuufahamisha na kuukumbusha umma wa Tanzania kuwa inao utaratibu wa kuwasaidia wafanyabiashara kwa kutoa ushauri wa kitaalamu unaojulikana kama TAE(Technical Assistance to Exporters) na kupima bidhaa ili kuwawezesha kusafirisha nje ya nchi (export) bidhaa zilizokidhi matakwa ya viwango vya nchi zinapokwenda na kuepusha bidhaa zao kurudishwa kwa kutokidhi viwango vya nchi husika au viwango vya kitaifa.

TBS inatoa huduma hii ili kuwawezesha wafanyabiashara kusafirisha bidhaa zenye ubora ambao ndio msingi wa viwanda vya kesho. Mpaka sasa kuna wafanyabiashara ambao wamefaidika na mfumo huu na tungependa kuona wafanyabiashara   wengi zaidi wakifaidika.

Tunapenda kutoa wito kwa wafanyabiashara wote kutumia fursa hii na kufuata utaratibu huu ili kuhakikisha bidhaa zao zina ubora nazinakidhi matakwa ya Viwango vya nchi zinapokwenda.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Shirika la Viwango Tanzania (TBS)
S.L.P. 9524, Dar es Salaam
Simu: +255 222450298/2450206/2451763-6
Hotline: 0800 110 827
Email: .(JavaScript must be enabled to view this email address)
Tovuti: http://www.tbs.go.tz

Kwa maelezo zaidi fungua hapa

TAARIFA_KWA_UMMA.pdf