TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAJI YA KUNYWA YA DEW

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ni Shirika la Umma lililoanzishwa upya kwa Sheria ya Viwango Na.2 ya mwaka 2009. Jukumu kubwa la Shirika chini ya Sheria hii ni kuandaa viwango vya kitaifa na kusimamia utekelezaji wake.

Hivi karibuni kumekuwa na taarifa mitandaoni zikienea kuwa kuna maji yanayoitwa DEW yameingia nchini kupitia njia zisizo rasmi kutoka Nigeria na kuwa maji hayo yana vijidudu vya kueneza ugonjwa wa ebola na yameshaua watu zaidi ya 180 huko Nigeria. Taarifa hiyo imeambatana na taarifa kwa umma iliyotolewa na Shirika la Viwango (TBS), miaka iliyopita ikitolea ufafanuzi juu ya jambo hilo.

TBS inawataka wananchi kutotilia maanani taarifa hizo kwani ni taarifa za uzushi na hazina   ukweli wowote. Hapa nchini kuna maji yanayozalishwa mkoani Rukwa yanayoitwa DEW Drop ambayo huzalishwa na kiwanda cha Dew Drop Drinks Co.Ltd Maji haya yalithibitishwa ubora wake na kupewa leseni tangu tarehe 2013-08-23 na mara ya mwisho kukaguliwa ili kuthibitisha ubora wake ilikuwa 2016-08-02 na maji hayo yanakidhi ubora wa kiwango TZS 574. 

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linapenda kuwakumbusha kwa mara nyingine kutumia bidhaa zilizothibitishwa na TBS ili kuhakikisha usalama kwa mtumiaji.


Kwa taarifa zaidi wasiliana na:

Mkurugenzi Mkuu
Shirika la Viwango Tanzania
S.L.P. 9524
Dar es Salaam
Tel: +255-22- 2450206
Hotline:0800110827
E-mail: .(JavaScript must be enabled to view this email address)
Tovuti:www.tbs.go.tz


Tafadhali bonyeza linki ifuatayo ili uweze kupakua tangazo hili:


tangazo_dew.pdf