TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Shirika la viwango Tanzania limekuwa likifanya ukaguzi wa kushtukiza wa bidhaa zilizopo sokoni na viwandani mara kwa mara, lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa bidhaa hizo zinakidhi matakwa ya kiwango cha bidhaa husika wakati wote. TBS kwa kushirikiana na Taasis ya Nishati Jadididu (TAREA) iliamua kufanya ukaguzi wa kushtukiza kufuatia malalamiko mengi kuhusiana na ubora wa Vipande vya umeme nuru katika soko la Tanzania ili kutatua tatizo. Mnamo tarehe 23-06-2015, TBS ilifanya ukaguzi wa Umeme Nuru (Solar Power panels) katika maeneo yafuatayo;

Keko- Mwanga, Mtaa wa Msimbazi, Mtaa wa Congo. TBS ilibaini baadhi ya wasambazaji walikuwa na bidhaa za umeme nuru zilizo chini ya kiwango nyingi zikitokea nchini China.
Jumla ya vipande vya umeme nuru 1321 kutoka duka na ghala la Regal Solar Ltd vilizuiwa kuuzwa; na 164 kutoka duka la Nishati Electronics Ltd pia vilizuiwa kuuzwa baada ya ubora wake kutiliwa shaka mpaka matokeo ya maabara yatakapotoka. Na vile vile wakaguzi walichukua sampuli kutoka duka la Keoali Power & Equipments Co.Ltd.

Matokeo ya maabara yalitoka na kuonesha kuwa sampuli hizo zilizochukuliwa katika maduka tajwa zimefeli.

Tafadhali bonyeza linki ifuatayo kwa maelezo zaidi:

press_conference_-_solar_panel.pdf