TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU NAFASI ZA AJIRA

Mnamo tarehe 07.06.2017 limetoka tangazo la kazi linalosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu nafasi za ajira zilizotangazwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Shirika linachukua nafasi hii kukanusha taarifa hiyo na kusihi umma kuipuuza taarifa hiyo ambayo siyo ya kweli. Tangazo la kazi linalosambaa ni la mwaka 2015 ambalo lilitangaza nafasi za ajira kupitia tovuti na magazeti mbalimbali katika kipindi hicho

Tunaomba umma wa Watanzania ufahamu kuwa Shirika la Viwango Tanzania lina utaratibu maalumu wa kutangaza nafasi za ajira kupitia vyombo rasmi vya habari pamoja na tovuti ya Shirika na si vinginevyo.

Hivyo basi nafasi za ajira zikitokea zitatangazwa kwa utaratibu tajwa na sio kwenye mitandao ya kijamii kama ilivyosambazwa taarifa hii.


 
Kwa maelezo zaidi wasiliana na:

Mkurugenzi Mkuu
Shirika la Viwango Tanzania
S L P 9524
DAR ES SALAAM
Simu: +255 22 2450206
Hotline: 0800 110 827
Nukushi: +255 22 2450959
Baruapepe: .(JavaScript must be enabled to view this email address)


Tafadhali bofya hapa kwa maelezo zaidi:

TAARIFA_KWA_VYOMBO_VYA_HABARI_KUHUSU_NAFASI_ZA_AJIRA_.pdf