Taarifa kwa Waagizaji na Wakala wa Forodha

imageKibali cha muda cha bidhaa kutoka nje ya nchi

Shirika la Viwango Tanzania linapenda kuwafahamisha waagizaji na wakala wa forodha kuwa limetayarisha kibali cha muda (Provisional Permit for entry of imported goods) cha kupakia kwenye mfumo wa TANCIS ambacho kitatumika badala ya fomu ya awali ya “Destination Inspection Request Form.” Dhumuni la kibali hicho ni kumruhusu wakala wa forodha kuendelea na taratibu za forodha kabla TBS haijakamilisha taratibu za ukaguzi.

Wakala wa forodha kwa niaba ya waagizaji wanatakiwa kuzingatia yafuatayo:

1. Kwa mizigo iliyokaguliwa nchi ilipotoka chini ya mpango wa “Pre-shipment Verification of Conformity to standards programme (PVoC)”, wakala wa forodha anatakiwa apakie kwenye TANCIS cheti cha ubora (CoC). CoC ipakiwe kwenye TANCIS mara tu ikishapokewa kutoka kwa wakala wa ukaguzi wa TBS yaani Societe Generale de Surveillance (SGS), China Certification & Inspection Group Co. Ltd (CCIC) au Bureau Veritas (BV).

2. Kujaza fomu ya kibali cha muda kwa bidhaa zinazotakiwa zikaguliwe zikifika hapa nchini. Fomu hiyo inapatikana kwenye tovuti ya TBS (http://www.tbs.go.tz). Wakala wa forodha atatakiwa kupakia kibali cha muda kwenye mfumo wa TANCIS ili aweze kuendelea na taratibu za forodha na kupata hati ya tathmini (assessment document).

3. Baada ya kupata hati ya tathmini, taratibu za ukaguzi na upimaji wa bidhaa zitaendelea kama kawaida kwa wakala wa forodha kuwasilisha nyaraka za mzigo kwenye ofisi ya TBS iliyopo Diplomat House katika makutano ya mitaa ya Mkwepu na Kaluta, Dar es Salaam. Utaratibu huu na mabadiliko madogo yaliyofanywa utaanza rasmi tarehe 2018-02-05.

ANGALIZO: Wakala wa forodha atakayefanya kinyume na utaratibu huu au kutoa taarifa ya uongo atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria zilizopo.


Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na:

Mkurugenzi Mkuu
Shirika la Viwango Tanzania
S.L.P 9424
Dar esSalaam.
Simu: +255 (022) 2450206/+255 (022) 2450298
Baruapepe: .(JavaScript must be enabled to view this email address)
Hotline:0800110827


Tafadhali bofya linki ifuatayo ili uweze kupakua tangazo hili na fomu ya ukaguzi wa mizigo nchini:

KIBALI_CHA_MUDA_CHA_BIDHAA_KUTOKA_NJE_YA_NCHI.pdf

PROVISIONAL_TBS_CERT._-_col_-_kiambatisho_A.pdf