TAARIFA KWA WAAGIZAJI NA WAUZAJI WA VILAINISHI MITAMBO NA MAGARI (LUBRICANTS OIL)

Shirika la Viwango Tanzania linapenda kuwataarifu waagizaji na wauzaji wa vilainishi hapa nchini kwamba limefanyia marekebisho ya viwango vya kitaifa ya vilainishi vya mitambo na magari na bidhaa zinazohusiana.

Viwango hivyo ni kama vifuatavyo;

TZS 647:2014 Engine oils-Minimum performance-Specification
TZS 667:2014 Motor vehicles brake fluids-Specification
TZS 675:2014 Multipurpose automative gear lubricant(EP)-Specification

Hivyo basi waagizaji na wauzaji wote wa vilainishi wanatakiwa kuzingatia viwango vilivyorekebishwa ili kukidhi matakwa ya viwango hivyo . 
Kwa yeyote atakayeshindwa kutekeleza agizo hili hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake kwa mujibu wa sheria ya viwango namba 2 ya mwaka 2009.

Kwa taarifa hii shirika linatoa muda wa mwezi mmoja kuanzia tarehe 07 Januari 2016 hadi tarehe 07 februari2016 kwa waagizaji na wauzaji kuthibitisha ubora wa bidhaa hizo.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:

Mkurugenzi Mkuu,
Shirika la Viwango Tanzania
S.L.P.9524,
Dar Es Salaam
DAR ES SALAAM.

Simu: +255 22 245 0298,245 0206,245 0949
Nukushi: +255 22 245 0959
Barua pepe:  .(JavaScript must be enabled to view this email address)


Tafadhali bonyeza linki ifuatayo ili uweze kulipata tangazo hili:

TAARIFA_KWA_WAAGIZAJI_NA_WAUZAJI_WA_VILAINISHI_MITAMBO_NA_MAGARI_(LUBRICANTS_OIL).pdf