TAARIFA KWA WAAGIZAJI NA WAZALISHAJI WA VILAINISHI VYA MITAMBO NA MAGARI

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ni Shirika la umma lililoanzishwa kwa Sheria ya Viwango Na.2 ya mwaka 2009. Jukumu kubwa la Shirika, chini ya Sheria hii ni kuandaa viwango vya kitaifa na kusimamia utekelezaji wake.

Hivi karibuni kumekuwa na uingizwaji na uuzwaji wa vilainishi vya mitambo na magari ambavyo ni bandia na chini ya kiwango, hali ambayo inaathiri ufanisi wa mitambo na injini za magari, hivyo kuathiri uchumi wa nchi.
Kutokana na hali hiyo, Shirika la Viwango la Tanzania (TBS) litafanya kikao na waagizaji, wazalishaji na wauzaji wa vilainishi vya mitambo na magari tarehe 2016-04-12, katika ofisi za TBS zilizopo Ubungo, kuanzia saa 03.00 asubuhi. Wadau wote mnahimizwa kuthibitisha ushiriki wenu kabla ya tarehe 2016-04-09, kwa kutumia baruapepe .(JavaScript must be enabled to view this email address) au Hotline +0800110827.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:

Mkurugenzi Mkuu,
Shirika la Viwango Tanzania,
S.L.P. 9524,
Dar es Salaam,
Simu: +255(022) 2450206
Hotline: +0800110827
Barua pepe: .(JavaScript must be enabled to view this email address)
Tovuti: http://www.tbs.go.tz

Tafadhali bonyeza linki ifuatayo hapa chini kupata hili tangazo

TANGAZO-KISWAHILI.pdf