TAARIFA KWA WAAGIZAJI WA BIDHAA KUTOKA NJE YA NCHI

image
Shirika la Viwango la Tanzania (TBS) hivi karibuni limebaini uwepo wa wimbi la udanganyifu kwa baadhi ya waagizaji wakubwa wa bidhaa kutoka nje ya nchi ambao wamekuwa wakikwepa kukaguliwa bidhaa zao na mawakala wa ukaguzi wa TBS ambao ni “Societe Generale de Surveillance” (SGS), “Bureau Veritas” (BV) na China Certification & Inspection(Group) Inspection Co Ltd’’(CCIC) na kulazimika kufanyiwa ukaguzi hapa nchini.

Chini ya utaratibu wa ukaguzi wa bidhaa huko zinakotoka “Pre-shipment Verification of Conformity to Standards”(PVoC) bidhaa zinazoruhusiwa kukaguliwa hapa nchini ni zile zenye thamani isiyozidi dola za Kimarekani 5000 na endapo shehena itakuwa na thamani juu ya hapo, mwagizaji hulipishwa faini ya asilimia kumi na tano (15%) ya thamani ya shehena,usafirishaji na dhamana (CIF).
Waagizaji hawa wa bidhaa wamekuwa wakifanya udanganyifu wa thamani ya bidhaa wanazoziingiza kuwa chini ya dola za Kimarekani 5000 ili kukwepa kulipa faini pale wanapokuwa hawajafanya ukaguzi huko zinakotoka.
Kutokana na udanganyifu huo Shirika linawahimiza waagizaji wa bidhaa kuhakikisha kuwa bidhaa zao zinakaguliwa na mawakala wa TBS kabla ya kuingiza nchini ili kuepukana na kutozwa faini na kukaguliwa nchini.
Shirika kwa mara nyingine linawataarifu kuwa ifikapo tarehe 2017-10-01, waagizaji wa bidhaa watakaoingiza bidhaa bila kukaguliwa na kudanganya thamani halali ya bidhaa watatozwa faini kulingana na thamani ya shehena iliyoanishwa na TRA (TRA Assessed CIF Value) 

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
Mkurugenzi Mkuu,
Shirika la Viwango Tanzania(TBS),
S.L.P. 9524,
Dar es Salaam,
Simu: +255(022) 2450206
Hotline: +0800110827
Barua pepe: .(JavaScript must be enabled to view this email address)
Tovuti: http://www.tbs.go.tz

Kwa maelezo zaidi bofya hapa

TAARIFA_KWA_WAAGIZAJI_WA_BIDHAA_KUTOKA_NJE_YA_NCHI.pdf