TAARIFA KWA WAAGIZAJI WOTE WA BIDHAA KUTOKA NJE YA NCHI

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ni Shirika la umma lililoanzishwa kwa Sheria ya Viwango No.2 ya mwaka 2009. Jukumu kubwa la Shirika chini ya Sheria hii ni kuandaa viwango vya kitaifa na kusimamia utekelezaji wake.

Shirika linapenda kuwakumbusha waagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi kuwa wanapaswa kukagua bidhaa zao kwa wakala wa TBS walioko katika nchi husika kabla ya kuziingiza nchini. Yeyote asiyejua taratibu za uingizaji wa bidhaa nchini anashauriwa kutembelea tovuti ya Shirika http://www.tbs.go.tz/index.php/services/category/pre-shipment_verification_of_conformity au kuwasiliana na Shirika kwa maelezo Zaidi. Shirika halitakubaliana na utetezi wowote utakaotolewa kwa sababu ya kutokujua taratibu.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu,
Shirika la Viwango Tanzania,
S.L.P. 9524,
Dar es Salaam,
Simu: +255(022) 2450206
Hotline: +0800110827
Barua pepe: .(JavaScript must be enabled to view this email address)
Tovuti: http://www.tbs.go.tz