TAARIFA KWA WAUZAJI, WASAMBAZAJI NA WAZALISHAJI WA MABATI

image
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kushirikiana na Tume ya Ushindani (FCC) wanawataarifu wauzaji, wasambazaji wazalishaji na wananchi wote kuwa kumekuwa na tabia ya wauzaji na wasambazaji kufuta taarifa kamili za mabati yaani “Marking”.

Suala hili limebainika katika ukaguzi wa pamoja uliofanyika tarehe 2017-08-30 na TBS,FCCna jeshi la polisi kuwa kampuni ya Verox Enterprises Ltd iliyopo Buguruni Madenge/Chama ambao ni wauzaji na wasambazaji wa mabati, inafanya uchakachuaji kwa kufuta alama sahihi ya utambulisho kwenye bidhaa ya mabati na kubadilisha unene wa mabati (gauge) na kuandika unene usiosahihi kwa lengo la kuwadanganya wanunuaji wa bidhaa hiyo ili kujipatia faida zaidi.Mfano gauge 32 inabadilishwa na kuandikwa gauge 30, Ufutaji huu hufanyika zaidi kwenye mabati ya gauge 32 ili kuwadanganya wanunuaji kuwa ni gauge 30.Vilevile gauge30 hufutwa na kuuzwa kama gauge 28.
Hivyo basi TBS na FCC wanawaonya wauzaji, wasambazaji na wazalishaji wa bidhaa ya mabati kuwa ni kosa kubadilisha au kuandika taarifa za uongo katika bidhaa ili kujipatia faida isiyostahili.  Kwa yeyote atakaebainika anafanya uchakachuaji/udanganyifu huo ,atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Kwa maelezo zaidi bofya hapa chini.
TANGAZO_LA_MABATI.pdf