TAARIFA KWA WAZALISHAJI WA NONDO

UTAMBULISHO WA AINA ZA NONDO NA LEBO

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ni Shirika la Umma lililoanzishwa upya kwa Sheria ya Viwango Na. 2 ya mwaka 2009. Jukumu kubwa la Shirika chini ya Sheria hii ni kuandaa viwango vya kitaifa na kusimamia utekelezaji wake. Mapema mwaka jana (2015), TBS ilifanyia marekebisho kiwango cha nondo, TZS 142 (Sehemu ya 2):2015 na kuongeza matakwa ya kuweka utambulisho wa aina za nondo na lebo. Aidha, Shirika lilitoa muda wa mwaka mmoja kwa wazalishaji kujiandaa kabla ya utekelezaji wa kiwango hiki (TZS 142 (Sehemu ya 2):2015).
Baada ya kuisha kwa kipindi hicho cha maandalizi, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) sasa linapenda kuwaasa wazalishaji wote wa nondo kuhakikisha kuwa bidhaa zao zinawekewa utambulisho wa aina za nondo na lebo kuanzia 2016-03-01.

Kwa taarifa zaidi wasiliana na:

Mkurugenzi Mkuu
Shirika la Viwango Tanzania
S L P 9524
Dar es Salaam
Tel: +255-22- 2450206
Hotline: 0800110827
Baruapepe: .(JavaScript must be enabled to view this email address)
Tovuti: http://www.tbs.go.tz

Tafadhali bonyeza linki ifuatayo ili uwe kulipata tangazo hili

TAARIFA_KWA_WAZALISHAJI_WA_NONDO.pdf