TANGAZO KWA WAAGIZAJI BIDHAA KUTOKA NJE YA NCHI NA MAWAKALA WA FORODHA

Katika kuhakikisha taratibu za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zinazofanyika katika mfumo wa TANCIS haziathiriwi na shughuli za uingizaji wa vibali vya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) katika mfumo huo, mawakala wa forodha wenye dhamana ya waagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi wanatakiwa kuzingatia yafuatayo:

1. Kuweka vyeti halisi vya ubora wa bidhaa husika (Certificate of Conformity (CoC)) katika mfumo wa TANCIS. Zoezi hili ni kwa bidhaa zinazoingizwa nchini kupitia mfumo wa ukaguzi wa nje ya nchi (Pre-shipment Verification of Conformity (PVoC)). Cheti cha ubora (CoC) husika kitaingizwa katika mfumo huo mara tu mwagizaji bidhaa atakapopokea cheti hicho kutoka kwa mmoja wa mawakala wa TBS ughaibuni, yaani Societe Generale de Surveillance (SGS), China Certification & Inspection Group Co. Ltd (CCIC) au Bureau Veritas (BV).

2. Kujaza fomu ya maombi ya ukaguzi kwa bidhaa zinazoingizwa nchini kupitia mfumo wa ukaguzi wa ndani ya nchi wa TBS (Destination Inspection (DI)). Fomu hiyo inapatikana katika tovuti ya TBS (http://www.tbs.go.tz). Baada ya kuijaza, fomu hiyo iingizwe katika mfumo wa TANCIS kama kiambatisho. Vile vile fomu hiyo itatumika badala ya barua ya maombi ya ukaguzi wa ndani ya nchi (DI), kama ilivyokuwa ikifanyika.

3. Baada ya kupata ripoti ya tathmini kutoka TRA, taratibu nyingine za uhakiki wa vyeti na ukaguzi zitaendelea kama zinavyofanyika sasa katika jengo la Diplomat, makutano ya mitaa ya Mkwepu na Kaluta jijini Dar es Salaam. Utekelezaji wa tangazo hili unaanza tarehe 2016-11-28.

ANGALIZO: Wakala yeyote wa forodha atakayekiuka maelekezo haya na kuingiza nyaraka nyingine tofauti katika mfumo wa TANCIS atawajibishwa kwa mujibu wa sheria.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:


Mkurugenzi Mkuu
Shirika la Viwango Tanzania (TBS)
S L P 9524
Dar es Salaam
Tanzania
Simu: +255 22 2450298/+255 22 2450206
Barua pepe: .(JavaScript must be enabled to view this email address)


Tafadhali bonyeza linki zifuatayo ili uweze kupakua tangazo hili na fomu ya kuomba kuingiza bidhaa zinazotoka nje:


TanzazoTANGAZO_KWA_CFA_-_NOVEMBER_2016_(1).pdf

Fomu ya kuomba kuingiza bidhaa zinazotoka nje (Imports Application Form):Destination_inspection_Request_.pdf