TANGAZO LA MWISHO KWA WAAGIZAJI WA BIDHAA KUTOKA NJE YA NCHI WALIONGIZA MAKONTENA BILA KUKAGULIWA

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linawataka mawakala walioingiza makontena nchini bila kukaguliwa na TBS kujisalimisha mara moja kufuatia agizo la Waziri lililowapa siku nne kujisalimisha lakini bado mpaka sasa hawajatekeleza agizo hili. Ikumbukwe kuwa ukaguzi wa bidhaa hizo ni wa lazima ili kumhakikishia ubora mtumiaji au mlaji wa mwisho.

Shirika lilitoa agizo kwa wafanyabiashara walioingiza makontena bila kukaguliwa na TBS kufika katika ofisi za TBS ili kupata huduma ya ukaguzi ndani ya siku 4, kuanzia tarehe 14 hadi tarehe 18 Octoba, 2016 zilizotolewa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mheshimiwa Charles Mwijage (Mb).  Mpaka sasa kuna baadhi ya wafanyabiashara ambao hawajajitokeza kwa ajili ya taratibu za ukaguzi, wafanyabiashara hao ni kama walivyoorodheshwa katika jedwali lifuatalo:

Tafadhali bonyeza linki ifuatayo ili uweze kuona orodha ya wafanyabiashara ambao hawajajitokeza katika ofisi za TBS kwa ukaguzi:

TANGAZO_LA_MWISHO_KWA_WAAGIZAJI_WA_BIDHAA_KUTOKA_NJE_YA_NCHI_WALIONGIZA_MAKONTENA_BILA_KUKAGULIWA-1.pdf