TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA UDEREVA - NAFASI 2

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linakaribisha maombi ya nafasi za kazi ya udereva, kutoka kwa watanzania wenye sifa zinazotakiwa ili kujaza nafasi za udereva. Ajira hii ni ya mkataba wa kipindi cha miezi mitatu.

A .SIFA ZA MUOMBAJI

Muombaji anatakiwa kuwa na cheti cha kuhitimu kidato cha nne (CSE) au kidato cha sita (ACSE), awe na leseni ya udereva daraja “C” ya uendeshaji na uelewa mzuri wa alama za barabarani pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka mitatu bila kusabisha ajali (suala hili litafuatiliwa katika kitengo cha usalama barabarani).Sambamba na hilo Muombaji anatakiwa kuwa na cheti cha majarabio ya ufundi daraja la III pamoja na cheti cha udereva mahiri daraja la pili kutoka chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)

B. MAJUKUMU YA KAZI

• Kuendesha gari la shirika
• Kutunza na kuandika daftari la safari “ log- book” kwa safari zote
• Kufanya uchunguzi wa gari kabla ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo
• Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari
• Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote
• Kutekeleza kazi nyingine yoyoye atakayopangiwa na mkuu wake wa kazi

C. MASHARTI YA JUMLA KWA MUOMBAJI

• Muombaji awe raia wa Tanzania
• Muombaji awe na umri usiozidi miaka 35
• Barua zote ziambatanishwe na vyeti husika na maelezo binafsi ya muombaji (CV).
• Barua zote ziwe na anwani ya uhakika na namba za simu za kuaminika.
• Maombi yote yatumwe kwa anwani ifuatayo kabla ya tarehe 17 Disemba 2012.KAIMU MKURUGENZI MKUU
SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA
S.L.P 9524
DAR ES SALAAM
TANZANIA

Tangazo hili pia linapatikana kwenye tovuti ya TBS http://www.tbs.go.tz