TBS blocks substandard gas oil consignment

Tanzania Bureau of Standards (TBS) has blocked 5,000 metric tonnes of gas oil (diesel) destined for the local market, for safety reasons.The consignment arrived at the Dar es Salaam Port on 13th June, 2011 from the United Arab Emirates aboard MT. Gulf Jumeirah and the consignee has been identified as Addax Energy SA.

TAARIFA KWA UMMA - KUZUIWA KWA SHEHENA YA MAFUTA KUINGIA NCHINI

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limezuia shehena ya mafuta ya dizeli yenye ujazo wa tani 5,000 kuingia nchini.

Shehena hiyo iliwasili katika Bandari ya Dar es Salaam Juni 13, 2011 kwa meli ya MT. Gulf Jumeirah ikitokea Falme za Kiarabu na kampuni iliyoagiza mzigo huu inajulikana kwa jina la Addax Energy SA.
TBS ilipima sampuli ya mafuta hayo kutoka kwenye shehena hiyo na kubaini kuwa halijoto ya mwako (flash point temperature) ya mafuta hayo haikidhi matakwa ya kiwango cha Tanzania 674:2009, Automotive diesel fuel – Specification.

Matokeo ya vipimo yalionesha kuwa halijoto hiyo ya mwako ni 56 oC wakati kiwango kinataja 66 oC.

Halijoto ya mwako inahusiana na uwezo wa mafuta kulipuka au kutolipuka endapo utatokea mtikisiko wowote hususan wakati wa usafirishaji. Ni kigezo muhimu sana katika kutathmini ubora wa mafuta kwani kutokidhi kigezo hiki kunaweza kusababisha maafa.

Halijoto ya mwako ni muhimu sana katika usalama, hususan wakati wa usafirishaji wa mafuta.

Waagizaji wote wa mafuta wanapaswa kuhakikisha kuwa mafuta yote yanayoingizwa katika soko la Tanzania yanakidhi matakwa ya viwango vya kitaifa.

Katika hatua nyingine, TBS inamsaka mwagizaji wa pombe kali aina ya GORDON’S ambayo imezagaa sana mjini Moshi ili aweze kuelimishwa matakwa ya kiwango cha bidhaa hiyo.

Pombe hiyo imepimwa ubora wake na TBS na kuonekana kwamba inakosa maelezo muhimu kwenye vifungashio, mfano tarehe ya kutengenezwa pamoja na “batch number”. Tunahisi kwamba pombe hii imeingizwa nchini kupitia njia zisizo halali.

Charles M Ekelege
Mkurugenzi Mkuu - Shirika la Viwango Tanzania