Je Viwango vina manufaa gani
Viwango ni zana yenye nguvu sana kwa kusaidia ubunifu na kuongeza tija. Uwekaji viwango wenye ufanisi je unakuza ushindani na kuongeza faida. Viwango vinaiwezesha kampuni:
a)Kukuvutia na kujihakikishia wateja
b)Kuonesha uongozi wa soko
c)Kujenga kumusu ushindani
d)Kujenga na kudumisha kanuni bora
e)Kuzingatia sheria za taifa
Viwango ni zana yenye nguvu sana katika soko. Kutimiza Viwango vya Tanzania ni njia inayofaa zaidi ya kujipambanua au kujitofautisha katika soko lenye ushindani. Aidha, kutengeneza bidhaa au kutoa huduma zinazotimiza viwango vinavyohusika huzidisha uwezo wao ukilinganisha na zile zinazotolewa au kutengenezwa na wengine, na vivyo kuongeza uwezekano wa mauzo na kukubalika zaidi katika maeneo mbalimbali. Kasdri walaji wanavyoelewa vizuri kuhusu uchaguzi wao, utimizaji viwango vinavyotambuliwa unazidi kuwa muhimu.
Viwango ni alama ya ubora inayoheshimika, alama za uthibitisho huzinufaisha zaidi biashara za bidhaa na taratibu zinazothitibisha kutimiza viwango vnavyohusika. Alama hizi (Kama vile Alama za Viwango vya ubora Tanzania) hutambuliwa kwa urahisi na kuwa kama alama ya ubora, usalama na utendaji.
Viwango vinaweza kuimarisha miundombinu. Uwekaji viwango unaweza kuleta manufaa yanayopimika vinapotumiwa ndani ya miundombinu ya kampuni yenyewe. Mawasiliano yenye ufanisi kwenye mnyororo wa ugavi na kuwapo kwa vyombo vya kisheria kunaleta biashara nzuri na ongezeko la wateja. Gharama za biashara na mashaka vinaweza kupunguzwa, michakato ya ndani kuimarishwa na mawasiliano kuboreshwa.
Uwekaji viwango unakuza mifumo kushirikiana hasa katika kuleta uwezo wa ushindani zaidi na unatakiwa kwa ajili ya biashara ya bidhaa na huduma yenye ufanisi.