Je, ISO ni nini
Je, ISO ni nini
Shirika la Uwekaji Viwango la Kimataifa ni mtayarishaji mkubwa Duniani na mchapishaji wa Viwango vya Kimataifa. ISO ni mtandao wa taasisi za viwango za kitaifa za nchi 162, mwanachama mmoja kwa kila nchi, ina sekretarieti Kuu, Geneva Uswisi inayoratibu mfumo. ISO ni shirika lisilo la kiserikali linalokuwa kiungo baina ya sekta za umma na za binafsi. Hivi sasa kamati mbalimbali za kiufundi za TBS huchangia mawazo na maoni kwa uwekaji viwango vya Kimataifa kwa kupitia kwenye kamati mbalimbali za kiufundi za ISO.