Je, TBS ni nini?
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) shirika la umma, chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara. Taasisi hii ya viwango ya Taifa la Tanzania iliyoanzishwa na Serikali kama sehemu ya jitihada ya kuimarisha miundombinu kwa sekta za viwanda na biashara kwenye uchumi nchini. Shirika hili lilianzishwa kwa sheria ya Bunge Na.3 ya Mwaka 1975 kama Taasisi ya Viwango ya Taifa na kuanza rasmi kazi tarehe 16 Aprili, 1976. Baadaye ilibadilishwa jina na kuwa Shirika la Viwango Tanzania kwa Sheria Na.1 ya Mwaka 1977. Tarehe 20 machi 2009, sheria ya viwango Na. 3 mwaka 1975 ilitanguliwa na kubadilishwa na Sheria ya Viwango Na. 2 ya Mwaka 2009.
Na.2 Shirika hili limeanzishwa kama sehemu ya jitihada za Serikali ili kuimarisha miundombinu saidizi ya kitaasisi kwa sekta za viwanda na biashara za uchumi. TBS ina mamlaka na wajibu wa kudhibiti ubora wa bidhaa za aina mbalimbali, kuhimiza uwekaji wa Viwango, kuhimiza uzingatiaji viwango, usalama, tathmini ya uzingatiaji viwango na kufanya vipimo katika sekta ya Viwanda na Biashara. Aidha, ifahamike kuwa TBS ni mwanachama wa Shirika la Uwekaji Viwango la Kimataifa (ISO) na Shirika la Vipimo na Mizani la Kimataifa (BIPM).