SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA(TBS)
e-Services

Mauzo ya Viwango

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linatoa huduma ya mauzo ya Viwango vya Tanzania (TZS), Viwango vya Afrika Mashariki (EAS), Viwango vya Afrika (ARSO) na Viwango vya Kimataifa (ISO) kwa wateja wa ndani na nje ya Tanzania.

Iwapo unahitaji kiwango, unaweza kuwasiliana nasi kwa kutembelea ofisi ya TBS iliyo karibu nawe, kupiga simu ya bure 0800110827 au kutuma barua pepe kupitia standardssales@tbs.go.tz.

Bei za Viwango

Bei za viwango zinapatikana katika Katalogi ya Viwango iliyopo kwenye tovuti hii.

Taarifa Zinazohitajika ili Kununua Kiwango

Mteja anaombwa kuwasilisha taarifa zifuatazo kuwezesha mchakato wa uandaaji wa Namba ya Malipo (Control Number).

- Jina kamili la kampuni au mtu binafsi:                                       (Lazima)

- Barua pepe:                                                                                    (Lazima)

- Namba ya simu:                                                                             (Lazima)

- Namba ya Kiwango, Jina la Kiwango au aina ya bidhaa anayotaka kuzalisha       (Lazima)

- Mahali ulipo (Mkoa/Mji na Nchi)                                                  (Lazima)

Tafadhali hakikisha kuwa taarifa zilizotolewa ni sahihi ili kurahisisha mchakato wa malipo na upokeaji wa kiwango.

Baada ya malipo kuthibitishwa, kiwango husika kitatumwa kwenye barua pepe ya mteja.

 

Huduma kwa Watafiti na Wanafunzi

Maktaba ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) iliyopo Ubungo, Dar es Salaam, ni rasilimali muhimu kwa ajili ya tafiti za kitaaluma, ubunifu, maendeleo ya bidhaa pamoja na masomo yanayohusisha ubora na usalama.

Kupitia Maktaba hii, watafiti, wanafunzi na wanataaluma wanaweza kupata taarifa zinazohusiana na viwango pamoja na nyaraka mbalimbali za rejea kwa ajili ya kusoma na kufanya marejeo ndani ya Kituo.

Watafiti, wanafunzi na wanataaluma wanakaribishwa kutumia rasilimali zinazopatikana katika Kituo hiki ili kuongeza maarifa yao na kusaidia shughuli za utafiti katika nyanja mbalimbali za sayansi, teknolojia, viwanda na biashara.



Settings