SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA(TBS)
e-Services

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limepokea tuzo na utambuzi kadhaa wa hadhi ya juu kutokana na utendaji wake bora wa usimamizi wa viwango na mchango wake katika kuhakikisha ubora, usalama wa umma, na ubunifu katika utoaji wa huduma kwa umma.

TUZO NA UMAHIRI

NA. TAREHE AINA YA TUZO/UMAHIRI MTOAJI
1.

2022-03-28

Taasisi ilipata Ithibati ya kimataifa (accreditation) katika  Uthibitishaji wa mifumo (System Certification) kwa kiwango cha ISO 17021-1.

SADCAS

2.

2023-07-11

Taasisi Bora ya Udhibiti Barani Afrika kwa mwaka 2023.

The African Business Leadership Awards (UK)

3.

2023 -08-18

Tanzania kupita TBS ilifanikiwa kuwa katika ngazi ya nne kati ya tano katika tathmini ya kuangalia kiwango cha utekelezaji wa kanuni za afya kimataifa katika eneo la usimamizi wa usalama wa chakula

Shirika la Afya Duniani (WHO)

4.

2023-09-22

ISO Next Generation, iliyotambua mchango wa wataalam TBS katika kuandaa viwango vinavyochagiza maendeleo endelevu ya kimataifa (UN SDGs)

Shirika la Viwango Duniani (ISO)

5.

2024-09-16

Taasisi ya kwanza katika Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kupata ithibati (accreditation) ya mifumo ya udhibiti ubora wa bidhaa (Product Certification) ya kimataifa katika wigo mpana (wide scope) ndani ya muda mfupi na ni ya taasisi ya tatu kupata ithibati hiyo katika SADC.

SADCAS

6.

2025-10-15

Taasisi ya kwanza Tanzania na ya pili Afrika Mashariki kupata Ithibati ya umahiri katika mifumo ya ukaguzi kwa kiwango cha kimataifa (ISO:17020)

SADCAS

7.

2025-11-25

Taasisi ya kwanza katika Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kupata Ithibati ya umahiri wa mfumo wa usimamizi wa chakula katika kiwango cha kimataifa toleo jipya (ISO 22003:2022)

SADCAS

8.

2025-12-03

Taasisi inayoibukia katika Ufuatiliaji wa Usugu wa Vimelea dhidi ya Dawa (AMR) katika Usalama wa Chakula

African Center for Disease Control and Prevention (AfricaCDC) and African Union Commision IBAR (AU IBAR)

9.

2025-12-16

Taasisi Bora ya Udhibiti nchini Tanzania

Public Service Innovation Awards

10.

2026-02-02

Taasisi ya pili katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kutambulika uwezo wake wa vipimo kimataifa kwa kuchapisha machapisho 18 (17 ya jotoridi na 1 la ujazo)

 Shirika la Vipimo Duniani (BIPM)

11.

2026-05-27

TBS Ilitambulika kwa Mchango wake Katila Elimu Jumuishi

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam- Mlimani.

12.

2026-06-03

Taasisi ya Tatu Katika Kuimarisha Usimamizi wa Utawala na Rasilimali watu katika Utumishi wa Umma

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

13.

2026-06-30

Taasisi Bora ya udhibiti Afrika Mashariki

East Africa Public Services Awards

14.

2026-06-30

Taasisi Bora ya Tatu ya Serikali iliyofanya maabdiliko makubwa kwenye utendaji (year to year improvement) pamoja na kuongeza gawio kwenye mfuko wa Serikali kwa mwaka wa 2025/2026.

Msajili wa Hazina

15.

2026-07-31

Taasisi ya pili afrika Mashariki na ya saba Afrika kuoanisha mfumo wa udhibiti ubora wa Nchi na wa Bara la Afrika.

 ARSO

Utambuzi huu unaakisi juhudi za pamoja za Bodi, Uongozi na wafanyakazi wote wa TBS katika kuhakikisha kuwa bidhaa zilizopo sokoni zinakidhi viwango vinavyohitajika na ni salama kwa walaji. Hii inaimarisha sifa ya TBS kitaifa, kikanda na kimataifa, na kufungua fursa za ushirikiano zaidi na washirika wa kimataifa.



Settings