Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
The TBS Management Systems Certification Body offers Certification services on the following International Standards:
a) ISO 9001:2015 Quality Management Systems (QMS);
b) ISO 22000:2018 Food Safety Management Systems (FSMS);
c) HACCP - Hazard Analysis and Critical Control Points;
d) ISO 21001:2018 Educational Organization Management Systems (EOMS);
e) ISO 14001:2015 Environmental Management Systems (EMS);
f) ISO 45001:2018 Occupational Health and Safety Management Systems (OH&SMS); and
g) ISO 50001:2018 Energy Management System.
TBS Management Systems Certification Body is a Body under Tanzania Bureau of Standards (TBS) that provides an assessment based around the chosen standard of an organization e.g. ISO 9001, ISO 14001, ISO 45001 etc.
The Certification Body will award a certificate to organizations to show that they have complied with the requirements set out in the standard.
Wajasiriamali wanaoanza, wadogo wadogo na wa Kati, hasa wanaokuzwa na Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO) au wanaotambuliwa na Serikali wanapata huduma za uthibitisho bure. MSMEs hao hawatakiwi kulipa ada yoyote ya uthibitisho wa bidhaa zao. TBS pia inawafundisha MSMEs katika mikoa mbalimbali kuhusu uzalishaji bora na salama..
Alama za viwango ni kwa bidhaa zinazotengenezwa nchini. Kwa bidhaa zinazoagizwa nje ya nchi, TBS inatoa hati kwa bidhaa zilizofanyiwa vipimo vya TBS. Mlaji yeyote mwenye shaka kuhusu ubora wa bidhaa hizo au hapana anaweza kuuliza kwenye ofisi za TBS au kupitia namba ya Simu ya bure 0800110827. Mlaji pia anahimizwa kutafuta alama za ubora za nchi zinakotoka bidhaa hizo.
Muda halali wa hati ni mwaka mmoja tu, kila mwisho wa mwaka, mteja anatakiwa kuomba kuongezewa muda kuhakikisha kuwa kila mteja aliyesajiliwa ananafasi katika ngazi ya kisheria kukaguliwa mara moja kwa mwaka, endapo kwa bahati mteja hakukaguliwa baina vya vipindi hivyo.
Ndiyo, TBS inafanya ukaguzi kila siku na kukusanya Sampuli. Ukaguzi wa bechi bandarini, viwanja vya Ndege, Vituo vingine vya kuingia nchini na kwenye ghala za waagizaji bidhaa. TBS Pia hufanya ukaguzi wa uchunguzi mara kwa mara kwa wateja wenye leseni za kutumia alama ya “tbs” na wale waliosajiliwa chini ya mpango wa uthibitisho wa bidhaa zilizopimwa. Ukaguzi wa kabla ya kupewa leseni/ hati waombaji wapya katika mpango wa “tbs” na uthibitisho wa bidhaa zilizopimwa pia wanafanyiwa ukaguzi.
Kwa kampuni zilizosajiliwa, TBS hufanya ukaguzi takribani mara nne kwa mwaka. Ukaguzi wa kwanza hufanywa kiwandani baada ya kupokea ombi la uthibitisho kutoka kwa mteja. Baada ya uthibitisho, TBS hufanya ukaguzi angalau mara tatu, ama kwenye maghala au mahali anaponunua bila mzalishaji kujua. Ukaguzi hufanywa hivyo kuhakikisha kuwa bidhaa zinatimizwa viwango wakati wote.
Utambuzi rassmi ni tathmini ya utimizaji viwango ya taasisi zinazotoa huduma za tathmini ya utimizaji viwango. Ni mchakato unataka kuona uthibitisho wa ustadi, mamlaka au uaminifu. Maabara mbalimbali za TBS zimetambuliwa rasmi na SADCAS dhidi ya ISO/ IEC 17025, Masharti ya jumla kwa ajili ya ustadi wa maabara na alama za vipimo.
Mchakato wa uthibitisho unaanza na maombi ya mzalishaji kwa Mkurugenzi Mkuu. Baada ya maombi kupokewa na Mkurugenzi Mkuu, mzalishaji anajibiwa na kuelezwa taratibu zote muhimu za kufuata kwa ajili ya uthibitisho. Mara nyingi au kama kawaida mzalishaji anatakiwa apate viwango utoka TBS kabla ya kuanza mchakato wote. Ni lazima ifahamike kuwa uthibitisho hufanywa dhidi ya kiwango mahususi; kwa hiyo ni lazima kupata kiwango kwanza.
Uthibitisho ni uhakikisho unaofanywa na mtu mwingine kuwa bidhaa, huduma, mtu au mfumo wa usimamizi unatimiza masharti yaliyoelezwa. Kwa kumpa mununuzi Imani kwamba bidhaa au huduma inatimiza masharti, uthibitisho huwezesha biashara ndani ya nchi na baina ya nchi. Shirika la Viwango Tanzania linaedesha Mipango mine ya uthibitisho ambayo ni: Mpango wa uthibitisho wa alama ya TBS, Mpango wa Uthibitisho wa bechi kwa bidhaa zinazoingizwa nchini, Mpango wa uthibitisho wa bidhaa zilizopimwa, na mpango wa usajili wa mifumo ya usimamizi.
Viwango vyote vya Tanzania vinaweza kununuliwa kutoka kwenye maktaba ya TBS au mtandaoni kwa kutumia TBS web store katika tovuti ya TBS kwenye Menyu ya Huduma Mtandao. Mkusanyiko wote wa viwango vilivyochapishwa unaweza kutafutwa kwenye tovuti ya TBS katika katalogi ya viwango vya TBS kwenye menyu ya Menyu ya uwekaji viwango vinavyokubaliwa (Standardization). Unaweza kutafuta jina, namba ya kiwango, bidhaa, au uainishaji wa kimataifa wa namba ya kiwango (ICS)