Upimaji

Shirika la viwango Tanzania (TBS) ina nyumba ya upimaji bora inayopima sampuli mbalimbali za bidhaa.Nyumba ya upimaji ilianzishwa mwaka 1982 kwa ajili ya:


a)Kuwasaidia watengenezaji kuongeza ubora wa bidhaa zao

b)Kutoa nyenzo kwa ajili ya upimaji wa bidhaa na kuhakikisha bidhaa inafaa kwa matumizi yaliyokusudiwa

c)Kuhakiki ubora wa bidhaa kabla ya kusafirishwa nje ya nchi na kabla ya kuingizwa nchini

Nyumba ya upimaji ya TBS pia hutoa nyenzo za upimaji haraka, sahihi na siri kwa ajili ya upimaji wa bidhaa,ushauri wa kiufundi na maelekezo kuhusu njia za upimaji na mafunzo ya maabara kwa watumishi

TBS ina maabara mahususi 9:

1.Maabara ya kemia

2.Maabara ya kemia ya chakula

3. Maabara ya Mikrobiolojia

4.Maabara ya nguo na ngozi

5.Kituo cha teknolojia ya ufungashaji

6.Maabara ya najengo na ujenzi

7.Maabara ya uhandisi makanika

8.Maabara ya uhandisi umeme

9.Maabara ya metrolojia

Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma za upimaji tafadhali bofya hapa:

https://tbs.go.tz/pages/test-house

Kwa taarifa zaidi kuhusu taratibu za upimaji, tafadhali bofya kiungo kifuatacho:

sample testing procedure