Uidhinishaji wa Mifumo ya Usimamizi
Mpango wa Usajili Mifumo ya Usimamizi
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linatoa uidhinishaji mifumo ya usimamizi kulingana na masharti ya viwango yva kimataifa kwa kampuni za umma na za binafsi watengenezaji na watoa huduma wengine mawanda ya uidhinishaji mifumo ya usimamizi inahusu
| ISO 9001 | Mifumo ya Usimamizi wa ubora |
| ISO 14001 | Mifumo ya Usimamizi wa Mazingira |
| ISO 45001 | Mifumo ya Usimamizi wa Afya na Usalama kazini/mahala pa kazi |
| TZS 1770 | Uchambuzi wa hatari na maeneo muhimu ya uthibiti |
Manufaa ya uidhinishaji wa mfumo wa usimamizi
a. Kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kwa kuwa michakato yako ypote itakuwa imepangwa na kueleweka na kila mtu kwenye biashara au shirika. Hali hiyo inaongeza tija na ufanisi kupunguza gharama za ndani.
b. Hutimiza masharti muhimu ya kisheria na usimamizi
c.Hupanuka kwenye masoko mapya, kwa sababu baadhi ya sekta na wateja wanahitaji ISO 9001 kabla ya kufanya biashara.
d.Hubainisha na kushughulikia mashaka ya inayohusiana na shirika lako.
e.Huboresha humjali mteja au kufahamu mchakato ndani ya kampuni
f.Huboresha dhamira ya usimamizi na kufanya uamuzi
g.Hali bora Zaidi ya kazi kwa kufanya kazi.
h.Huongeza motisha kwa wafanyakazi
i.Hupunguza ngharama za dosari za ndani na za nje
j.Kuendelea kuimarisha mifumo ya usimamizi wa ubora
k.Kuboresha takwimu/sifa ya kampuni
l.Huongeza imani ya mteja
Tafadhali fungua link zifuatazo kuona watoa huduma au Kampuni walioidhinishiwa Mifumo yao ya Usimamizi:
certified firms under iso 9001 2015 qms 2025 03 19
certified firms under haccp 2025 03 19
certified firms under iso 14001 2015 environment management system 2023 08 04
certified firms under iso 45001 2018 occupational health and safety management system 2023 08 04