Katalojia ya Viwango
Katalojia ya Shirika ya Viwango Tanzania (TBS) ina taarifa za zaidi ya viwango vya Tanzania (TZS) 2,000, vya hiari na vya lazima.
Viwango hivyo ni vya maeneo mbalimbali kama vile uhandisi wa umeme, uhandisi wa mitambo, uhandisi wa ujenzi, mazingira, kilimo na chakula, ufungashaji, uwekaji wa lebo/utambulishi, nguo, uzalishaji, teknolojia za habari na mawasiliano, nishati, usimamizi wa ubora, tathmini ya utimizaji kanuni na huduma.
Kumbukumbu zilizomo kwenye katalojia zina taarifa kuhusu jina la kiwango, namba ya kiwango (TZS ...), idadi ya kurasa na wigo. Viwango vinaainishwa kulingana na mfumo wa Kimataifa wa uainishaji wa Viwango (ICS).
Tafadhali bofya kiungo cha hapa chini kupata katalojia: