TANZANIA BUREAU OF STANDARDS(TBS)
e-Services

Viwango vya Lazima

Kiwango kinachochapishwa na kutangazwa na Waziri mwenye dhamana ya Viwanda na Biashara kuwa ni cha lazima baada ya kupitia hatua zote za uendelezaji viwango. Kiwango cha lazima kinaeleza masharti ya lazima au sifa bainifu muhimu yanayohitajika kuhakikisha kufaa kwa bidhaa fulani. Masharti ya viwango vya lazima yamejumuishwa kwenye kanuni za kitaalamu/ kiufundi.

Bidhaa daima inapohusu kuathiri afya, usalama, mazingira au athari kubwa kwa uchumi wa taifa, kiwango kama hicho huchapishwa kama kiwango cha lazima. Viwango vingine vyoteukiacha vilivyoelezwa hapo juu, vinatambuliwa kuwa ni viwango vya hiari.

Orodha ya viwango vya lazima vilivyotangazwa kwenye gazeti la Serikali vinapatikana kwenye kiungo kifuatacho;

list of compulsory tanzania standard

 

 

 

 



Settings