SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA(TBS)
e-Services

TBS yawataka wazalishaji kuzingatia ubora

Reason Image

WAZALISHAJI wa bidhaa mbalimbali nchini wametakiwa kufuata taratibu za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili bidhaa zao ziweze kuwa bora na salama kwa walaji wao.

Wito huo ulitolewa kwa nyakati tofauti na Meneja Kanda ya Kusini (TBS) Bw. Abel Mwakasonda kwenye Maonesho ya Wakulima ambayo yalimalizika mwishoni mwa wiki kwenye  viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.

Alisema wazalishaji waliotembelea banda la TBS miongoni mwao walikuwa hawajasajili maeneo yao ya vyakula na vipodozi,hivyo walikaribishwa kufika kwenye banda la shirika hilo kupata elimu.  

"Kwa hiyo tangu Agosti mosi tulikuwa hapa kwa ajilii ya kutoa elimu na kuwakaribisha kupata elimu kwenye banda la TBS ili waweze kusaji  maeneo yao ya  biashara kwenye banda letu,"alisema.

Mwakasonda allisema washiki 
maonesho hayo wale wote ambao hawajasili maeneo walitakiwa kufika TBS kusajili maeneo yao.

Alisema huduma hiyo ilikuwa inatolewa kwema banda la TBS na wale waliokuwa na changamoto walipitiwa mwenye maeneo yao ili waweze kutatuliwa changamoto hizo.

"Kwa hiyo wake waliobahatika kupita banda la TBS mkoani Lindi  walipata elimu walizozihitaji, TBS inashauri wafanyabiashara na wazalishaji  kuzingatia ubora, iwe ni biashara za ujenzi, mavazi na vyakula ili waweze kupata taratibu kuzalisha bidhaa ambazo ni bora zaidi,"alisema.

Kwa upande wa wajasiriamali ambao mitaji yao  bado ni changamoto, alisema wao kama TBS wanathibitisha ubora wa bidhaa zao bure kwa gharama za Seríkali.

Alisema hata kwenye mabanda yao waliweza kuwafuata na kuwapa elimu ya usindikaji bora wa bidhaa wanazozisindika na kuzalisha,viwe ni vifaa vya ujenzi na vyakula."

Alisema watapata nafuu ya kuthibitishiwa ubora wa bidhaa zao kwa miaka mitatu bure.

Kwa wale wanaoagiza bidhaa zao nje.wawe wadogo au wakubwa, alisema wanashauriwa kuthibitisha ubora wake kabla hazijaingia nchini lengo likiwa ziendane na na takwa ya TBS, ili kulinda walaji na biashara zao zitakuwa salama zaidi.

"Lengo ni bidhaa zao ziweze kuendana na matakwa ya TBS,"alisema.

Alisema TBS ni ofisi ya Umma, hivyo wasiogope kwenda kupata elim



Settings