TBS hutoa mafunzo ya stadi muhimu katika maeneo ya uwekaji viwango na uhakiki wa ubora. Tangu ianzishwe mpaka sasa maelfu ya watumishi wa fani mbalimbali wamepewa mafunzo na idadi hiyo inazidi kuongezeka kila siku. Shirika pia linatoa huduma ya mafunzo ya kitaalamu kwa wateja wote.
Shirika limedhamiria zaidi kutoa maarifa si kitaifa tu bali kwa wadau ndani ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na wengine wanaopenda.
Yafuatayo ni maeneo ya kozi za mafunzo zinazotolewa hivi sasa:
a)ISO 9001: Mifumo ya Usimamizi wa Ubora
b)ISO/IEC 17025: Masharti ya jumla ya ustadi wa maabara za kupima na alama za vipimo
c)ISO 15189, Masharti ya ubora na ustadi kwenye maabara za kitabibu
d)ISO 22000: Mifumo ya Usimamizi wa Usalama wa Chakula
e)ISO 14001, Mfumo wa usimamizi wa mazingira.
f)ISO 1770, Mfumo wa Uchanganuzi wa hatari na Udhibiti wa maeneo muhimu (HACCP) – Masharti ya shirika lolote kwenye unyororo wa chakula
g) Semina za uhamasishaji, mafunzo na warsha kwa wajasiriamaliwanaoanza, wadogo wadogo na wa kati (MS MES) kuhusu uwekaji viwango vinanvyokubalika na uhakiki wa ubora na
h)Kozi nyingine za uwekaji viwango na uhakiki wa ubora wa matakwa ya mteja
Huduma za Ushauri na Uelekezi
TBS inasaidia mashirika yanayohitaji kutekeleza huduma za mifumo ya usimamizi katika maeneo yafuatayo: uandikaji mwongozo, taratibu, matriki za mashaka, upeo/mawanda, mchakato wa uendeshhaji, mipango ya ubora wa malengo kufanya uhakiki wa ndani, mapitio ya usimamizi na maengine yanayohusu masharti ya mfumo usimamizi.
Muda: Huduma za ushauri na uelekezi zinategemea mahitaji ya shirika.
Matokeo yanayotarajiwa: mwongozo wa mfumo wa usimamizi, taratibu rasmi za uendeshaji, mchakato wa uendeshaji uliyobainishwa (SOPs), matriki ya mashaka iliyoandikwa na taratibu za kupunguza, maelekezo ya kazi, fomu, mpango wa uhakiki wa ndani, malengo ya uhakiki, ripoti ya uhakiki wa ndani, mapitio ya matokeo ya usimamizi na mengine yanayohusu masharti ya mfumo wa usimamizi.