Je TBS inafanya ukaguzi kubaini bidhaa hafifu sokoni
Je TBS inafanya ukaguzi kubaini bidhaa hafifu sokoni

Ndiyo, TBS inafanya ukaguzi kila siku na kukusanya Sampuli. Ukaguzi wa bechi bandarini, viwanja vya Ndege, Vituo vingine vya kuingia nchini na kwenye ghala za waagizaji bidhaa. TBS Pia hufanya ukaguzi wa uchunguzi mara kwa mara kwa wateja wenye leseni za kutumia alama ya “tbs” na wale waliosajiliwa chini ya mpango wa uthibitisho wa bidhaa zilizopimwa. Ukaguzi wa kabla ya kupewa leseni/ hati waombaji wapya katika mpango wa “tbs” na uthibitisho wa bidhaa zilizopimwa pia wanafanyiwa ukaguzi.

Kwa kampuni zilizosajiliwa, TBS hufanya ukaguzi takribani mara nne kwa mwaka. Ukaguzi wa kwanza hufanywa kiwandani baada ya kupokea ombi la uthibitisho kutoka kwa mteja. Baada ya uthibitisho, TBS hufanya ukaguzi angalau mara tatu, ama kwenye maghala au mahali anaponunua bila mzalishaji kujua. Ukaguzi hufanywa hivyo kuhakikisha kuwa bidhaa zinatimizwa viwango wakati wote.