TANZANIA BUREAU OF STANDARDS(TBS)
e-Services
Msaada wa Kiufundi kwa Wasafirishaji Bidhaa Nje ya Nchi

Msaada wa kiufundi kwa wasafirishaji nje ya nchi (TE) ni huduma inayowapa wasafirishaji bidhaa nje ya nchi taarifa muhimu na ushauri wa kiufundi katika masoko ya nje ya nchi

Kwa kawaida masharti ya usafirishaji bidhaa nje ya nchi katika uhakiki wa ubora na tathimini ya utimizaji viwango yanachunguzwa na nchi zinazoagiza bidhaa nje ya nchi. Hata hivyo, Shirika la Viwango Tanzania linaarifu umma kwamba, litatoa msaada wa kiufundi kwa wasafirishaji bidhaa nje ya nchi wanaohitaji kusafirisha bidhaa mbalimbali kwenye EAC, Afrika na nchi nyingine duniani.

Programu hii imepangwa katika makundi matatu yafuatayo;

1.Kiasi kidogo (chini ya 5 kg kwa kila kitu)

2.Bidhaa zenye leseni/ zilizosajiliwa

3.Kiasi kikubwa cha bidhaa zisizosajiliwa

 

Utaratibu wa maombi

1.Kiasi kidogo cha bidhaa (Chini ya 5 kg kwa kila kitu)

Kwa makundi haya ya bidhaa kama vile sampuli, zawadi, vifaa binafsi chini ya 5 kg, wasafirishaji nje ya nchi ni lazima wasajili na kuwasilisha maombi yao mtandaoni kwenye linki https://oas.tbs.go.tz na maombi yatashughulikiwa mtandaoni. Gharama ya huduma hii ni sh. 30,000/=.

2.Bidhaa za kiasi kikubwa zilizosajiliwa

Maombi yanafanywa katika linki https://oas.tbs.go.tz mteja atatakiwa kuonesha mtengenezaji aliyesajiliwa na TBS na namba ya leseni ya bidhaa inayohusika wanayotaka kusafirisha nje ya nchi. Maombi haya hushughulikiwa bure.

3.Kiasi kikubwa cha bidhaa zisizosajiliwa

Mwombaji katika kundi hili anatakiwa awasilishe maombi yake kila mwaka kwa maandishi baadaye kwa Mkurugenzi Mkuu TBS na awasilishe kwenye ofisi ya karibu ya TBS. Barua hiyo itashughulikiwa na mteja na mteja atapewa gharama zitakazojumuisha upimaji na ukaguzi. Baada ya kulipa gharama zinazotakiwa, sampuli na upimaji utafanywa ili kuhakikisha ubora na hati ya kusafirisha bidhaa itatolewa kwa mteja.



Settings