TBS inaendesha mipango mitatu ya idhini ya utoaji bidhaa kutoka nje, mipango hiyo ni:
Alama za viwango vya uidhinishaji wa ubora, mpango wa uidhinishaji Bechi/Kundi na mpango wa uidhinishaji wa bidhaa iliyopimwa.TBS pia inaendesha mpango wa uidhinishaji mifumo.
Uidhinishaji Alama za Viwango
Mpango wa uidhinishaji Alama za Viwango inaruhusu makampuni ya watengenezaji ambazo bidhaa zao zimefuata viwango vya Tanzania kutumia Alama za Viwango vya ubora za TBS kwa bidhaa zao.Mpango huu unataka bidhaa ziwe zimetimiza viwango vya Tanzania vinavyohusika. Alama za viwango vya ubora ni alama ambalyo watengenezaji wanaweza kutumia kukuzia bidhaa zao na walaji wataitafuta kama Ushahidi wenye kutegemea mwonekano wa kwanza.
Alama ya viwango vya ubora vya ‘’TBS’’ kwenye bidhaa inaonesha kuwa sampuli za bidhaa zinapimwa mara kwa mara na kuthibitishwa na TBS kwa mujibu wa viwango vinavyohusika vya Tanzania.Alama za viwango vya ubora ni alama ya biashara inayomilikiwa na TBS. Leseni ya kutumia alama hiyo inayolewa kwa watengenezaji bidhaa wanaofuata masharti makali ya kuhakiki ubora wa taratibu za utoaji leseni ya alama ya viwango.Alama ya viwango ni ishara ya ubora wa bidhaa na inatoa uhakika kwa watengenezaji na wanunuzi kwamba bidhaa zinaweza kutumika kwa usalama na kuaminika.
Alama ya viwango vya ubora vya TBS inawezesha watu wanunue kwa kujiamini kwa upande mwingine, inalinda watengenezaji dhidi ya ushindaji wa bidhaa hafifu na kuwawezesha kuthibitisha kwenye soko kuwa bidhaa zao zinakidhi masharti yote yaliyoelezwa kwenye viwango.
Mpango wa uthibitisho wa Bechi ya Bidhaa kutoka nje ya nchi
Mpango wa uidhinishaji Bechi/Kundi kwa bidhaa zinazoingizwa nchini ni sehemu ya utekelezaji wa Tangazo la Serikali. Na. 672 la 1998 – Kanuni za lazima za viwango vya uidhinishaji Benki/Kundi kwa bidhaa zote zilizoko kwenye viwango vya lazima.
Katika mpango huu pia Shirika la Viwango linatekeleza uhakiki wa utunzaji viwango kabla ya usafirishaji wa bidhaa. (PVOC) kwa mpango wa viwango ambapo ubora wa bidhaa unathibitishwa kwenye nchi zao.
Mpango wa Uidhinishaji wa Bidhaa iliyopimwa
TBS inaendesha mpango wa uidhinishaji wa bora wa bidhaa iliyopimwa ambapo mtengenezaji anadai kuzalisha kwa mujibu wa viwango vya kimataifa au vya nje vya Kampuni ambavyo havipatikani nchini Tanzania.Bidhaa ya utengenezaji hupimwa kwenye maabara ya TBS kwa mujibu wa viwango vinavyodaiwa kutumiwa na pia upimaji wa ukaguzi hufanywa inapoingia tu nchini kwa kuhakikisha ubora.
Mpango wa uidhinishaji wa bidhaa iliyopimwa ni mpango ambao TBS haikutoa kiwango cha bidhaa lakini hata hivyo kutimiza kiwango kinachotakiwa kama ilivyoainishwa na vipimo vya bidhaa na kuidhinishwa na kamati ya uidhinishaji vipimo ya TBS.
Mpango wa Usajili Mifumo ya Usimamizi
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linatoa uidhinishaji mifumo ya usimamizi kulingana na masharti ya viwanog yva kimataifa kwa kampuni za umma na za binafsi watengenezaji na watoa huduma wengine mawanda uya uidhinishaji mifumo ya usimamizi inahusu
ISO 9001
Mifumo ya Usimamizi wa ubora
ISO 14001
Mifumo ya Usimamizi wa Mazingira
ISO 45001
Mifumo ya Usimamizi wa Afya na Usalama kazini/mahala pa kazi
TZS 1770
Uchambuzi wa hatari na maeneo muhimu ya uthibiti
Manufaa ya uidhinishaji wa mfumo wa usimamizi
a.Kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kwa kuwa michakato yako yote itakuwa imepangwa na kueleweka na kila mtu kwenye biashara au shirika.Hali hiyo inaongeza tija na ufanisi punguza gharama za ndani.
b. Hutimiza masharti muhimu ya kisheria na usimamizi
c.Hupanuka kwenye masoko mapya, kwa sababu baadhi ya sekta na wateja wanahitaji ISO 9001 kabla ya kufanya biashara.
d.Hubainisha na kushughulikia mashaka ya inayohusiana na shirika lako.
e.Huboresha humjali mteja au kufahamu mchakato ndani ya kampuni
f.Huboresha dhamira ya usimamizi na kufanya uamuzi
g.Hali bora Zaidi ya kazi kwa kufanya kazi.
h.Huongeza motisha kwa wafanyakazi
i.Hupunguza ngharama za dosari za ndani na za nje
j.Kuendelea kuimarisha mifumo ya usimamizi wa ubora
k.Kuboresha takwimu/sifa ya kampuni
l.Huongeza imani ya mteja
TBS inaendesha mipango mitatu ya idhini ya utoaji bidhaa kutoka nje, mipango hiyo ni:
Alama za viwango vya uidhinishaji wa ubora, mpango wa uidhinishaji Bechi/Kundi na mpango wa uidhinishaji wa bidhaa iliyopimwa.TBS pia inaendesha mpango wa uidhinishaji mifumo.