Huduma Zinazotolewa na PTC
1. Upimaji wa Vifungashio na Malighafi zake
Kituo hupima ubora, uimara na uwezo wa vifungashio kulinda bidhaa wakati wa kuhifadhi, kushughulikia na kusafirisha bidhaa.
2. Mafunzo ya Teknolojia ya Ufungashaji
PTC hutoa mafunzo kwa viwanda na Biashara Ndogo na za Kati (SMEs) kuhusu mbinu bora za ufungashaji, uchaguzi wa malighafi na usanifu wa vifungashio vyenye ubora.
3. Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu
Kituo hufanya tafiti na kutoa ushauri kuhusu malighafi, teknolojia na usanifu wa vifungashio ili kusaidia biashara kupata suluhisho sahihi za ufungashaji.
4. Uthibitishaji wa Vifungashio
PTC hutoa huduma za uthibitishaji wa vifungashio na malighafi zake zinazokidhi viwango vinavyotumika na masharti husika ya uthibitishaji.
5. Kuwezesha Biashara ya Uagizaji na Uuzaji Nje ya Nchi
Kituo hutoa msaada wa kitaalamu kuhusu viwango na mahitaji ya vifungashio ili kuwezesha biashara ya malighafi za vifungashio na kusaidia upatikanaji wa masoko ya ndani na nje ya nchi.
6. Taarifa kuhusu Viwango na Teknolojia ya Ufungashaji
PTC hutoa taarifa na mwongozo kuhusu viwango, mahitaji ya kiufundi, aina za malighafi na teknolojia mpya za ufungashaji.