Kituo cha Taarifa na Maulizo (NEP)
NEP ni Kituo cha Taarifa na Maulizo kilichoanzishwa ndani ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kutokana na makubaliano yaliyofanyika kwenye Mkataba wa Vikwazo vya Kiufundi katika Biashara (TBT) wa Shirika la Biashara Duniani (WTO). Shabaha kuu ikiwa ni kusukuma mbele maendeleo ya Uchumi/biashara na kupunguza/kuondoa vizuizi vya biashara kati ya mataifa wakati tukilinda usalama wa wananchi, afya zao, wanyama, mimea, au mazingira. Kupitia huduma ya bure ya mtandaoni (ePing) https://www.epingalert.org/ ya Shirika la Biashara Ulimwenguni (WTO), NEP hutoa kwa wadau na umma taarifa za rasimu zilizoandaliwa juu ya:-
- Kanuni za Kisheria (Technical Regulations): Masharti ya lazima yanayosimamia sifa za bidhaa (kama vile lebo za chakula au viwango vya usalama vya vifaa vya kielektroniki).
- Viwango (Standards): Kanuni zinazoelezea/ainisha sifa au ubora wa bidhaa.
- Taratibu za Uthibitisho (Conformity Assessment): Hatua zinazochukuliwa kuhakikisha kuwa bidhaa inakidhi viwango vinavyotakiwa kama vile ukaguzi na upimaji wa bidhaa.
Huduma ya taarifa ya barua pepe ya ePing inaruhusu watumiaji waliojiandikisha kupokea taarifa za SPS/TBT zinazowavutia mahususi kulingana na vigezo kama vile bidhaa zinazojumuishwa au masoko ya nje. Inalenga kuziba pengo hilo na kutoa taarifa kwa wakati kuhusu mabadiliko ya Vikwazo vya Kiufundi vya Biashara (TBT) na mahitaji ya Usafi na Usafi wa Mazingira (SPS) kutoka kwa washirika wa biashara hadi wazalishaji, wauzaji bidhaa nje, Serikali na watumiaji wengine wanaovutiwa.
Wadau mbalimbali kama wazalishaji wa bidhaa, wauzaji bidhaa ndani na nje ya nchi, watoa huduma za kibiashara, Wafanyabiashara wadogo, wa kati, na Wakubwa, mashirika ya Serikali na binafsi, mashirika ya kimataifa, wanazuoni na taasisi za utafiti hupata taarifa kwa wakati kupitia ePing bila malipo.
NEP ina majukumu yafuatayo;-
- Kuifahamisha Sekretarieti ya WTO kuhusu utekelezaji unaokuja wa kanuni mpya/zilizorekebishwa za kiufundi (Masharti ya lazima yanayosimamia sifa za bidhaa, Kanuni zinazoelezea/ainisha sifa au ubora wa bidhaa, hatua zinazochukuliwa kuhakikisha kuwa bidhaa inakidhi viwango vinavyotakiwa)
- Kutayarisha taarifa kuhusu yaliyo hapo juu
- Kupakua na kusambaza taarifa za kigeni kwa wadau wa ndani
- Kujibu maswali kuhusu kanuni za kiufundi, viwango, na taratibu za tathmini ya ulinganifu
- Kukusanya na kusambaza taarifa ya mpango kazi wa kila mwaka kwa kituo cha habari cha ISO/IEC
Mauzo ya Viwango
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linatoa huduma ya mauzo ya Viwango vya Tanzania (TZS), Viwango vya Afrika Mashariki (EAS), Viwango vya Afrika (ARSO) na Viwango vya Kimataifa (ISO) kwa wateja wa ndani na nje ya Tanzania.
Iwapo unahitaji kiwango, unaweza kuwasiliana nasi kwa kutembelea ofisi ya TBS iliyo karibu nawe, kupiga simu ya bure 0800110827 au kutuma barua pepe kupitia standardssales@tbs.go.tz.
Bei za Viwango
Bei za viwango zinapatikana katika Katalogi ya Viwango iliyopo kwenye tovuti hii.
Taarifa Zinazohitajika ili Kununua Kiwango
Mteja anaombwa kuwasilisha taarifa zifuatazo kuwezesha mchakato wa uandaaji wa Namba ya Malipo (Control Number).
- Jina kamili la kampuni au mtu binafsi: (Lazima)
- Barua pepe: (Lazima)
- Namba ya simu: (Lazima)
- Namba ya Kiwango, Jina la Kiwango au aina ya bidhaa anayotaka kuzalisha (Lazima)
- Mahali ulipo (Mkoa/Mji na Nchi) (Lazima)
Tafadhali hakikisha kuwa taarifa zilizotolewa ni sahihi ili kurahisisha mchakato wa malipo na upokeaji wa kiwango.
Baada ya malipo kuthibitishwa, kiwango husika kitatumwa kwenye barua pepe ya mteja.
Huduma kwa Watafiti na Wanafunzi
Maktaba ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) iliyopo Ubungo, Dar es Salaam, ni rasilimali muhimu kwa ajili ya tafiti za kitaaluma, ubunifu, maendeleo ya bidhaa pamoja na masomo yanayohusisha ubora na usalama.
Kupitia Maktaba hii, watafiti, wanafunzi na wanataaluma wanaweza kupata taarifa zinazohusiana na viwango pamoja na nyaraka mbalimbali za rejea kwa ajili ya kusoma na kufanya marejeo ndani ya Kituo.
Watafiti, wanafunzi na wanataaluma wanakaribishwa kutumia rasilimali zinazopatikana katika Kituo hiki ili kuongeza maarifa yao na kusaidia shughuli za utafiti katika nyanja mbalimbali za sayansi, teknolojia, viwanda na biashara.