Announcements
Posted On: Jan 08, 2026
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU TAHADHARI YA USALAMA WA MAZIWA MBADALA YA WATOTO WACHANGA (BABY FORMULA) AINA YA SMA
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linapenda kuutaarifu umma kuwa mnamo tarehe 06 Januari 2026, Kampuni ya Nestlé nchini Uholanzi (Netherlands) ilichapisha katika tovuti yake taarifa ya kusitisha na kuondoa sokoni matoleo (batches) kadhaa ya bidhaa ya maziwa mbadala ya watoto wachanga (baby formula) aina ya SMA katika soko la dunia (recall notice). Hatua hiyo imechukuliwa kutokana na tahadhari ya uwezekano wa kuwepo kwa sumu aina ya Cereulide.