Announcements
Posted On: Apr 30, 2024
MKUTANO KATI YA TBS NA WAZALISHAJI, WAINGIZAJI NA WASAMBAZAJI WA BIDHAA ZA VIPODOZI HAPA NCHINI TAREHE 3 MEI, 2024
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeandaa mkutano kati yake pamoja na wazalishaji, waingizaji na wasambazaji wa vipodozi hapa nchini kwa lengo la kukuza uelewa wa matakwa ya Viwango vya bidhaa hizo. Mkutano huo utafanyika siku ya Ijumaa tarehe 3 Mei, 2024 katika ofisi za TBS Makao Makuu, Ubungo Dar es Salaam kuanzia saa 3:00 Asubuhi mpaka saa 7:00 Mchana.