Announcements
Posted On: Jan 20, 2021
TAARIFA KWA WAAGIZAJI WA MAGARI KUTOKA NJE YA NCHI
SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA (TBS) 2021-01-20
TAARIFA KWA WAAGIZAJI WA MAGARI KUTOKA NJE YA NCHI
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linawataarifu waagizaji na wauzaji wa magari kutoka nje ya nchi kuwa kuanzia tarehe 01 mwezi Machi, 2021, utaratibu wa kukagua magarikutoka nje ya nchi utafanyika baada ya kuwasili hapa nchini (Destination Inspection).Hivyo,magari yote yatakayosafirishwa kuanzia tarehe tajwa hapo juu yatakaguliwa katika bandari yaDar-es-Salaam.
Kwa sasa TBS inakagua magari kutoka nje ya nchi kupitia mawakala watatu(3) kutoka Japan na mmoja(1) kutoka Dubai ambao mikataba yao itakoma hivi karibuni.
Hivyo vyeti vya ukaguzi vitakavyotolewa na mawakala tajwa kwa magari yatakayosafirishwa kuanzia tarehe 01 mwezi Machi, 2021 havitatambulika na TBS.
Aidha,magari yatakayopimwa bandarini na kutokidhi matakwa ya kiwango yatahitaji kufanyiwa matengenezo nje ya bandari na kisha kuletwa na kupimwa tena kwenye yadi ya UDA mkabala na Bandari ya Dar es salaam.
Shirika litaendelea kuhakikisha kuwa magari yote yaliyotumika nakuingizwa nchini yanakidhi matakwa ya kiwango cha magari yaliyotumika.
Kwa taarifa zaidi kuhusu utaratibu huu mpyausisite kuwasiliana na:-
Mkurugenzi Mkuu,
Shirika la Viwango Tanzania (TBS),
SLP 9524,
Dar es Salaam.
Simu: +255(022)2450298/Hotline: +0800110827