Announcements
Posted On: Jan 28, 2021
UFAFANUZI WA TAARIFA KWA WAAGIZAJI WA MAGARI KUTOKA NJE YA NCHI
2021-01-28
SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA (TBS)
UFAFANUZI WA TAARIFA KWA WAAGIZAJI WA MAGARI KUTOKA NJE YA NCHI
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linapenda kutoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa iliyotolewa tarehe 2021-01-21 juu ya ukaguzi wa magari kutoka nje ya nchi.Tunapenda kufafanua kwamba, kwa sasa TBS inaendelea kukagua magari kutoka nje ya nchi kupitia mawakala watatu (3) walioko Japan na mmoja (1) Dubai mpaka pale mikataba yao itakapokoma tarehe 28 Februari, 2021.
Hivyo, Shirika litaendelea kuvitambua vyeti vyote ambavyo vitatolewa na mawakala tajwa ambao maombi yao yatakuwa yamepelekwa na kulipiwa kwa mawakala hao kabla ya tarehe 01 Machi, 2021. Vyeti hivyo vitatambulika mpaka pale vitakapokwisha muda wake ambao ni miezi mitatu (3) tangu tarehe ya cheti kutolewa.
Aidha, Shirika halitatambua vyeti vyote ambavyo maombi yake yatakuwa yamepelekwa kwa mawakala baada ya tarehe 28 Februari, 2021.
Shirika linaendelea kusisitiza kwamba kuanzia tarehe 01 Machi, 2021, utaratibu wa kukagua magari kutoka nje ya nchi utafanyika baada ya kuwasili hapa nchini (Destination Inspection) na waagizaji wote watatakiwa wapeleke maombi TBS na si kwa mawakala.
Waagizaji wanashauriwa kutuma maombi yao wakiambatisha, pamoja na nyaraka nyingine, vyeti vifuatavyo: Certificate of Cancellation, Certificate of Registration, Radiation free certificate na Export certificate.
ANGALIZO: Magari yatakayotoka Japan na Dubai kabla ya ukomo wa mkataba na kuwasili nchini baada ya ukomo wa mikataba bila cheti cha CoC yatatozwa faini (penalty).
Kwa taarifa zaidi usisite kuwasiliana na: -
Mkurugenzi Mkuu,
Shirika la Viwango Tanzania (TBS),
S.L.P. 9524,
Dar-es-Salaam.
Simu: +255(022)2450298/Hotline: +0800110827
Barua pepe: info@tbs.go.tz/Tovuti: www.tbs.go.tz
malalamiko @tbs.go.tz