SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA(TBS)
e-Services

UKAGUZI WA UTEKELEZAJI WA SHERIA

Shughuli za ukaguzi kwa madhumuni ya utekelezaji wa sheria zinalenga kuondoa katika soko bidhaa zilizopigwa marufuku, zisizo salama, zisizokidhi matakwa ya viwango na zisizofaa kwa matumizi; zinazopatikana katika masoko ya kawaida na katika majukwaa ya kidijitali au biashara za kielektroniki.

Shughuli hizi zinalenga kuhakikisha uzingatiaji wa matakwa ya Viwango na Kanuni kwa kuzuia vitendo vinavyokiuka matakwa ya Sheria ambavyo vinaweza kuhatarisha afya ya jamii, kuathiri mazingira na kudhoofisha ustawi wa walaji kutokana na bidhaa na huduma zisizokidhi matakwa ya Viwango.

TBS imeimarisha shughuli za utekelezaji wa Sheria kwa kushirikisha wananchi kupitia Sera ya Ulinzi kwa Watoa Taarifa (Whistleblowers Policy). Aidha, wakati wa kutekeleza shughuli hizo, Shirika linaweza kushirikiana na Mamlaka nyingine za udhibiti za Serikali.

Kwa mujibu wa Sheria ya Viwango Sura 130 na Kanuni zake, TBS huchukua hatua mbalimbali za kiudhibiti ili kushughulikia ukiukwaji wa Sheria. Hatua hizo ni pamoja na:

  1. Kuzuia bidhaa zisizokidhi matakwa ya viwango na zisizofaa kwa matumizi, pamoja na kusimamia uteketezaji wake kwa mujibu wa taratibu husika;
  2. Kuelekeza urejeshwaji wa bidhaa hafifu kwa hiari au kwa lazima kutoka katika soko.
  3. Kutoa barua za onyo na maelekezo yanayotaka kuchukuliwa kwa hatua za marekebisho ili kurejesha uzingatiaji wa matakwa ya viwango na Sheria.
  4. Kuanzisha na kuendesha mashauri ya Kisheria dhidi ya Wakiukaji wa matakwa ya Viwango, Kanuni na Sheria.
  5. Kufanya mikutano ya kuhamasisha na kuimarisha uzingatiaji wa matakwa ya viwango na Sheria.
  6. Kutoa taarifa kwa Umma kuhusu hali ya uzingatiaji wa viwango na matakwa ya kisheria kwa bidhaa na huduma.


Settings