SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA(TBS)
e-Services

1.0 UTARATIBU WA USAJILI WA BIDHAA

TBS husajili bidhaa za vyakula na vipodozi zinazozalishwa nje ya nchi na kuingizwa nchini Bidhaa zinazokidhi viwango tu ndizo husajiliwa  kuruhusiwa kuingizwa nchini.

1.1 Hatua ya Kwanza - Maombi

Maombi ya usajili hufanyika katika mfumo wa kielektroniki unaopatikana katika tovuti ya TB (www.tbs.go.tz) kwenye kitufe cha Huduma mtanda (e-service) halafu maombi ya huduma kwa njia y mtandao (OAS).

Mwombaji hutakiwa kujisajili katika mfumo na kisha kuingiza taarifa za bidhaa anazotaka kusajili.

1.2 Hatua ya Pili - Malipo

Mwombaji hupewa gharama za kusajili bidhaa husika pamoja na namba ya kumbukumbu ya malipo ya serikali kupitia kwenye mfumo wa kielektroniki.

Baada ya malipo hutakiwa kuwasilisha sampuli katika ofisi za TBS.

1.3 Hatua ya Tatu - Tathimini

Bidhaa hufanyiwa tathimini na mwombaji atapewa mrejesho kupitia mfumo wa kielektroniki (OAS) kama bidhaa imekidhi vigezo au la.

1.4 Hatua ya Nne – Usajili

Bidhaa zinazokidhi vigezo husajiliwa na cheti cha usajili hutolewa kupitia mfumo wa kielektroniki.

2.0 UTARATIBU WA USAJILI WA MAJENGO

TBS husajili majengo/maeneo yanayohusika na biashara za vyakula na vipodozi kama machinjio, mabucha, maduka makubwa (supermarkets), maduka ya vyakula na vipodozi, wanaopika vyakula kwenye masherehe (caterers), mahoteli, migahawa, maghala na maeneo ya uzalishaji.

2.1 Hatua ya Kwanza - Maombi

Maombi ya usajili hufanyika katika mfumo wa kielektroniki unaopatikana katika tovuti ya TBS (www.tbs.go.tz) kwenye kitufe cha Huduma mtandao (e-service) halafu maombi ya huduma kwa njia ya mtandao (OAS).

Mwombaji hutakiwa kujisajili katika mfumo na kisha kuingiza taarifa za jengo analotaka kusajili na kuambatanisha namba ya TIN, picha za mchoro wa jengo, leseni ya biashara pamoja na ramani inayoelekeza jengo lilipo ili kuwezesha wakaguzi kulifikia.

2.2 Hatua ya Pili - Malipo

Mwombaji hupewa gharama za kulipia kulingana na aina ya shughuli anayofanya katika jengo husika pamoja na namba ya kumbukumbu ya malipo ya serikali kupitia mfumo wa kielektroniki.

2.3 Hatua ya Tatu - Tathimini

Baada ya malipo kufanyika Mkaguzi atafika kukagua jengo kulingana na vigezo vilivyowekwa ili kujiridhisha na kisha mwombaji atapewa mrejesh

2.4 Hatua ya Nne - Usajili

Jengo lililokidhi vigezo husajiliwa na cheti cha usajili hutolewa kupitia mfumo wa kielektroniki.



Settings