MPANGO WA UFUATILIAJI WA BIDHAA KATIKA SOKO
Mpango huu unatekelezwa kwa lengo la kufuatilia na kuhakikisha kuwa bidhaa na huduma zinazopatikana katika soko la Tanzania zinakidhi matakwa ya Viwango na Kanuni chini ya Sheria ya Viwango, Sura ya 130.
Ufuatiliaji wa usalama na ubora wa bidhaa katika soko hufanyika kwa kuzingatia Mpango wa Ufuatiliaji ulioandaliwa kwa utaratibu maalumu na unaozingatia tathmini ya vihatarishi, ambao hutekelezwa kote nchini kupitia Ofisi za Kanda.
TBS hutoa miongozo kwa wazalishaji, waagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi, wafanyabiashara na wadau mbalimbali kuhusu uzingatiaji wa matakwa ya Viwango, Kanuni na Sheria.