Shirika la viwango Tanzania (TBS) linatekeleza uhakiki wa utimizaji wa viwango vy bidhaa kwa ajili ya kudhibiti baadhi ya makundi ya bidhaa za matumizi kutoka nje ya nchi.
A. Uhakiki wa utumiaji viwango kabla ya usafirishaji wa bidhaa (PVOC)
Uhakiki wa utimizaji viwango kabla ya usafirishaji wa bidhaa ni utaratibu wa uhakikiwa utimizaji wa viwango unaotumiwa kuhakiki kama bidhaa zitakazoingizwa kutoka nje ya nchi zinatimiza viwango stahiki vya taifa kabla ya kusafirisha bidhaa.Ni utaratibu wa uhakiki wa utimizaji viwango kwa bidhaa mahususi katika nchi zinazosafirisha bidhaa nje. Utaratibu huu ni kwa mujibu wa kifungu 4(1) (s) cha Sheria Na 2 ya Viwango ya mwaka 2009
Kabla ya usafirishaji kuja Tanzania shehena zote zinazoshahiki PVOC ni lazima zipate hati za utoaji bidhaa forodhani na hati ya utimizaji viwango (COC) ambazo zikikosekana bidhaa zinazowasili kwenye Bandari za Tanzania zitakataliwa au kutozwa faini.
Uhakiki wa PVOC hufanywa na wakala nyingine zilizoidhinishwa, zinazofanya ukaguzi halisi ikijumuisha upimaji wa maabara, upitiaji wa nyaraka na ukaguzi wa viwanda pale ambapo ni muhimu.
Manufaa Muhimu
- Hulinda afya,usalama na ulinzi watumiaji
- Huzuia ushindani usio wa haki kutokana na bidhaa kutoka nje za viwango duni
- Huwezesha utoaji bidhaa forodhani
- Hutokomeza uteketezaji au gharama za kusafirisha tena nje bidhaa zenye viwango duni
- Huzuia Tanzania isiwe jalala la bidhaa duni
Kwa maelezo zaidi tafadhali pakua viambatanisho:
1. PVoC Certification Procedure
guideline for pvoc programme 2025
2. Regulated HS Codes under PVoC Programme
3. Regulated HS Codes under Used Motor Vehicles
vehicles hs codes 29 march 2025
4. TBS PVoC Partners Addresses
contact addresses of liaison offices for pvoc service providers for general goods
ccic contact list for pvoc programme china
intertek worldwide contact list for pvoc programme
sgs pca worldwide contact list for pvoc programme
tuv rheinland worldwide contact list for pvoc programme
5. Zones of PVoC Service Providers
list of contracted pvoc sevice providers and respective zones for general goods
6. Summarized PVoC Procedure
7. Contact Addresses of PVoC Partners of Used Motor Vehicles
worldwide contact addresses of pvoc service providers used motor vehicles
contracted zones of pvoc service providers for used motor vehicle
8. PVoC Procedure for Used Motor Vehicles
pvoc procedures for vehicles 2020
9. Exemptions under the PVoC Programme
pvoc exempted categories & criteria.final
B. Ukaguzi Baada ya Mizigo Kuwasili Nchini (D1)
Ukaguzi baada mizigo kuwasili nchini unalenga uhakiki wa utimizaji wa viwango kwa bidhaa zinazowasili nchini kutoka nje. Ukaguzi huu ni kwa orodha ya bidhaa zote zote lazima na bidhaa zilizoingizwa bila ya hati ya utimizaji viwango (COC) chini ya mpango wa PVoC
Kwa maelezo zaidi tafadhali pakua viambatanisho:
1. Compulsory List of the HS Codes
2. Procedure for the Clearance of General Good Regulated under Destination Inspections
3. DI Penati
Vitu vilivyopo chini ya PVoC vilivyoingizwa nchini bila ya hati ya utimizaji viwango ni lazima vitozwe adhabu. Maelezo ya adhabu ya shehena /mizigo yameambatanishwa hapa;
penalty for un inspected general goods regulated under pvoc programme 2025
penalty for un inspected used motor vehicles regulated under pvoc programme 2025
4. Ukaguzi Baada ya Magari yaliyotumika Kuwasili Nchini
Utaratibu wa kutoa magari yaliyotumika chini ya mpango wa ukaguzi baada mzigo kuwasili nchini umeambatanishwa hapa:
Ili uweze kuingia kwenye mfumo tumizi mtandaoni tafadhali bofya kiungo/link ifuatayo:
B. Msaada wa Kiufundi kwa Wasafirishaji Bidhaa Nje ya Nchi
Msaada wa kiufundi kwa wasafirishaji nje ya nchi (TE) ni huduma inayowapa wasafirishaji bidhaa nje ya nchi taarifa muhimu na ushauri wa kiufundi katika masoko ya nje ya nchi
Kwa kawaida masharti ya usafirishaji bidhaa nje ya nchi katika uhakiki wa ubora na tathimini ya utimizaji viwango yanachunguzwa na nchi zinazoagiza bidhaa nje ya nchi. Hata hivyo, Shirika la Viwango Tanzania linaarifu umma kwamba, litatoa msaada wa kiufundi kwa wasafirishaji bidhaa nje ya nchi wanaohitaji kusafirisha bidhaa mbalimbali kwenye EAC, Afrdika nan chi nyingine duniani.
Kwa taarifa zaidi bonyeza link ifuatayo:
Msaada wa Kiufundi kwa Wasafirishaji Bidhaa Nje ya Nchi